SERIKALI YAENDELEA NA UANDAAJI WA KANUNI ZA BIMA ZA KILIMO KULINDA WAKULIMA – Habari Mpya

Na Jordan Mbwambo WF, Dodoma Serikali imesema inaendelea kukamilisha mchakato wa uandaaji wa Kanuni za Bima za Kilimo ambazo zitasaidia kuongeza upatikanaji wa kinga kwa wakulima dhidi ya majanga yanayoathiri mazao, mifugo, misitu na sekta ya uvuvi nchini. Hayo yamebainishwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe.Laurent Luswetula (Mb), alipokuwa akijibu swali la…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

Na Jordan Mbwambo WF, Dodoma

Serikali imesema inaendelea kukamilisha mchakato wa uandaaji wa Kanuni za Bima za Kilimo ambazo zitasaidia kuongeza upatikanaji wa kinga kwa wakulima dhidi ya majanga yanayoathiri mazao, mifugo, misitu na sekta ya uvuvi nchini.

Hayo yamebainishwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe.Laurent Luswetula (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ilemela, Mhe. Kafiti William Kafiti, aliyetaka kujua wakati ambao Serikali itakamilisha Kanuni hizo ili kuongeza na kupatikana kwa kinga kwa wakulima na mazao mbalimbali.

Mhe. Luswetula alisema kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Fedha inaendelea na utafiti na maboresho katika Sekta ya Bima ya Kilimo ili kuhakikisha mfumo huo unakuwa shirikishi na wenye kuvutia uwekezaji kwa wadau wa ndani na nje ya nchi.

“Serikali inaendelea na utafiti kuhusu bima katika mnyororo wa kilimo (mazao, mifugo, misitu na uvuvi) ili pamoja na mambo mengine kuwa na Kanuni zinazovutia uwekezaji katika bima ya kilimo na kuweka mazingira wezeshi kwa wakulima ili kupata huduma za bima kwa urahisi na haraka”, alisema Mhe. Luswetula.

Aliongeza kuwa, Serikali inakusudia kuhakikisha kanuni hizo zinakuwa rafiki kwa wakulima na wakati huo huo zikichochea ushiriki wa sekta binafsi katika kutoa huduma za bima ya kilimo nchini.

Aidha, alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa sekta ya bima kuhakikisha mfumo huo unakuwa endelevu na unaonufaisha wakulima kwa upana zaidi.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports