SERIKALI YAFAFANUA VIGEZO VINAVYOTUMIKA KUTOZA KODI YA MAJENGO KUPITIA LUKU – Habari Mpya

Na. Jordan Mbwambo, WF, Dodoma, Serikali imefafanua vigezo vinavyotumika katika utozaji wa Kodi ya Majengo (Property Tax) kupitia Mfumo wa Mita za Umeme za LUKU, hatua inayolenga kurahisisha ukusanyaji wa kodi na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa mapato ya ndani. Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), alipokuwa…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

Na. Jordan Mbwambo, WF, Dodoma,

Serikali imefafanua vigezo vinavyotumika katika utozaji wa Kodi ya Majengo (Property Tax) kupitia Mfumo wa Mita za Umeme za LUKU, hatua inayolenga kurahisisha ukusanyaji wa kodi na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa mapato ya ndani.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Tinnar Andrew Chenge, aliyetaka kujua kigezo kinachotumiwa na Serikali katika kutoza Kodi ya Majengo kupitia Mfumo wa Mita za LUKU.

“Kwa sasa Serikali inatumia viwango mfuto katika kutoza kodi ya majengo kupitia mita za umeme za LUKU. Vigezo vinavyotumika kutoza kodi ya majengo kupitia LUKU ni nyumba ya kawaida ambayo inatozwa shilingi 18,000 kwa mwaka au shilingi 1,500 kwa mwezi na nyumba ya ghorofa ambayo inatozwa shilingi 90,000 kwa kila sakafu kwa mwaka au shilingi 7,500 kwa kila sakafu kwa mwezi,” alisema Mhe. Luswetula.

Aidha, alisema kuwa nyumba za nyasi, udongo, majengo ya huduma za jamii, ibada pamoja na nyumba zinazoishi wazee wenye umri wa miaka 60 na kuendelea hazitozwi Kodi ya Majengo isipokuwa pale majengo hayo yanapotumika kwa shughuli za biashara.

Mhe. Luswetula alisema kuwa utaratibu huo unalenga kuhakikisha mfumo wa utozaji kodi unaendelea kuwa rahisi, wenye ufanisi na unaozingatia makundi maalum yanayostahili msamaha kwa mujibu wa sheria.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports