MADINI YA MILIONI 993 YAFANYIWA MNADA TANZANITE EXCHANGE CENTRE – Habari Mpya

MADINI ya Tanzanite ya thamani ya zaidi ya shilingi milioni 993 yameuzwa kwenye minada miwili iliyofanyika hivi karibuni katika jengo la Tanzanite Exchange Centre mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara. Afisa madini mkazi Mirerani (RMO) George Kaseza, ameyasema hayo kwenye ziara ya Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Kenani Laban Kihongosi alipotembelea…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

MADINI ya Tanzanite ya thamani ya zaidi ya shilingi milioni 993 yameuzwa kwenye minada miwili iliyofanyika hivi karibuni katika jengo la Tanzanite Exchange Centre mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

Afisa madini mkazi Mirerani (RMO) George Kaseza, ameyasema hayo kwenye ziara ya Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Kenani Laban Kihongosi alipotembelea jengo hilo na kukagua akiwa ameongozana na viongozi wa mkoa na wilaya.

Kaseza amesema minada miwili ilifanyika hivi karibuni ambapo mnada wa kwanza wa mabroka ulifanyika Mei 15 mwaka 2026 kwa washiriki 84 na madini ya shilingi 271,270,100 yalinunuliwa.

“Mnada wa pili wa dealers ulifanyika Mei 21 mwaka 2026 na madini ya thamani ya shilingi 721,750,000 yalinunuliwa,” amesema RMO Kaseza.

Amesema jengo la Tanzanite Exchange Centre linamilikiwa na Halamshauri ya Wilaya ya Simanjiro ila linaendeshwa na Tume ya Madini kupitia ofisi yake.

Katibu wa NEC, Itikadi Uenezi na Mafunzo Kenani Laban Kilongosi amewapongeza watumishi wa ofisi ya RMO Mirerani kwa namna wanavyofanya kazi katika eneo hilo.

Kenani amesema tayari soko hilo limeanza kuonyesha matokeo chanya ya uwekezaji huo kutokana na mwitikio mkubwa wa wafanyabiashara na mafanikio ya minada iliyofanyika ndani ya muda mfupi tangu kuanza kutumika.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports