Sekta binafsi kubeba miradi mikubwa ya maendeleo

DODOMA:Serikali imepanga kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika kugharamia na kutekeleza miradi ya maendeleo, ikisema hatua hiyo ni muhimu katika kuharakisha ukuaji wa uchumi na kuongeza fursa za ajira nchini. Mkakati huo umeainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2026/27, ambao umeweka uwekezaji na biashara miongoni mwa sekta muhimu zitakazoongoza mageuzi ya uchumi.…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

DODOMA:Serikali imepanga kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika kugharamia na kutekeleza miradi ya maendeleo, ikisema hatua hiyo ni muhimu katika kuharakisha ukuaji wa uchumi na kuongeza fursa za ajira nchini.

Mkakati huo umeainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2026/27, ambao umeweka uwekezaji na biashara miongoni mwa sekta muhimu zitakazoongoza mageuzi ya uchumi.

Akiwasilisha mpango huo bungeni, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, alisema Serikali itaendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji ili kuvutia mitaji, teknolojia na utaalamu kutoka ndani na nje ya nchi.

Alisema ushiriki mkubwa wa sekta binafsi unatarajiwa kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo huku ukipunguza utegemezi wa fedha za umma.

Profesa Mkumbo alisema Serikali pia itaendelea kutafuta washirika wa biashara na uwekezaji katika masoko mbalimbali duniani ili kuimarisha uwezo wa uchumi wa taifa.

Kwa mujibu wa mpango huo, uwekezaji wa sekta binafsi unatarajiwa kuchochea uzalishaji katika sekta mbalimbali za uchumi, kuongeza mapato ya wananchi na kufungua nafasi zaidi za ajira.

Hatua hiyo inaendana na mkakati mpana wa Serikali wa kujenga uchumi unaotegemea zaidi uwekezaji, biashara na uzalishaji wa ndani kama msingi wa maendeleo endelevu ya taif

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports