MOROCCO YAIWEKEA NGUMU BRAZIL KOMBE LA DUNIA – Habari Mpya

Morocco imeanza Fainali za Kombe la Dunia kibabe baada ya kuikalia kooni Brazil,ikilazimisha sare ya bao 1-1. Mara ya mwisho kwa Brazil kuanza kwa sare kwenye mechi yake ya kwanza kwenye Kombe la Dunia ilikuwa Juni 3,1978 ilipotoa sare kama hiyo dhidi ya Sweden, kwenye fainali zilizofanyika nchini Argentina. Morocco imekuwa ya kwanza kupata bao…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

Morocco imeanza Fainali za Kombe la Dunia kibabe baada ya kuikalia kooni Brazil,ikilazimisha sare ya bao 1-1.

Mara ya mwisho kwa Brazil kuanza kwa sare kwenye mechi yake ya kwanza kwenye Kombe la Dunia ilikuwa Juni 3,1978 ilipotoa sare kama hiyo dhidi ya Sweden, kwenye fainali zilizofanyika nchini Argentina.

Morocco imekuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 21, kupitia Ismael Saibari akifunga bao safi la kiufundi, akipokea pasi ya kiungo wake Brahim Diaz.

Brazil maarufu kwa jina la Selecao, ikasawazisha bao hilo dakika ya 32 kupita s Vinicius Junior, akifunga bao zuri akitengenezewa pasi ya mwisho na Bruno Guimares.

Timu zote zimeonyesha kiwango kizuri kwenye mchezo huo huku makipa wakipa wakifanya kazi kubwa ya kuzima mashambulizi ambapo kipa wa Morocco Yassine Bounou ameokoa mashamulizi manne huku mwenzake Allison Becker akifanya hivyo mara mbili.

Brazil imeonyesha kiwango kizuri ikitawala umiliki wa mpira kwenye vipindi vyote lakini ikakosa makali ya kutengeneza mashambulizi makali na kuweza kuyatumia.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports