TVLA YAWATAKA WAFUGAJI KUONGEZA MWITIKIO WA CHANJO ZA MIFUGO – Habari Mpya

FARIDA MANGUBE MOROGOGO  Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Dkt. Stella Bitanyi, amewataka wafugaji nchini kuongeza mwitikio wa kuchanja mifugo dhidi ya magonjwa mbalimbali ili kuimarisha afya ya mifugo, kuongeza uzalishaji na kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu. Akizungumza Juni 18, 2026 mjini Morogoro katika…

admin Avatar

by

2 minutes

Read Time

FARIDA MANGUBE MOROGOGO 

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Dkt. Stella Bitanyi, amewataka wafugaji nchini kuongeza mwitikio wa kuchanja mifugo dhidi ya magonjwa mbalimbali ili kuimarisha afya ya mifugo, kuongeza uzalishaji na kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

Akizungumza Juni 18, 2026 mjini Morogoro katika kikao kati ya TVLA na timu ya Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP), Dkt. Bitanyi amesema mwitikio wa wafugaji wadogo katika chanjo za mifugo bado ni mdogo licha ya upatikanaji wa chanjo zinazozalishwa na TVLA.

Dkt. Bitanyi amesema kupitia mradi wa C-SDTP, elimu zaidi inapaswa kutolewa kwa wafugaji kuhusu umuhimu wa chanjo ili kusaidia kupunguza magonjwa ya mifugo na kuongeza tija katika uzalishaji.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kudhibiti ugonjwa wa tupa mimba (Brucellosis) na magonjwa mengine yanayoambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu, huku akiwahimiza wananchi kutumia maziwa salama na kuyachemsha kabla ya matumizi.

Amesema TVLA ina jukumu la kufanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo, kuzalisha chanjo, kufanya tafiti za kisayansi na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wafugaji ili kuimarisha afya na uzalishaji wa mifugo nchini.

Kwa upande wake, Mratibu wa Kitaifa wa C-SDTP, Lazaro Kapela, amesema mradi huo unatekelezwa katika mikoa minane ya Tanzania Bara na mikoa mitano ya Zanzibar kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafugaji wa ng’ombe wa maziwa.

Kapela amesema mradi huo unawekeza katika mbegu bora za mifugo, malisho, huduma za afya ya mifugo, miundombinu ya maji na vituo vya kukusanyia maziwa ili kuongeza uzalishaji na kuwahakikishia wafugaji masoko ya uhakika.

Ameongeza kuwa mradi huo wa miaka 10, ulioanza mwaka 2024 kwa gharama ya dola za Marekani milioni 231, unashirikiana na TVLA kuimarisha matumizi ya chanjo na huduma za kitaalamu kwa wafugaji.

Naye Afisa Mwandamizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa C-SDTP, Goodluck Masawe, amesema mradi unatarajiwa kunufaisha kaya 140,000 sawa na zaidi ya watu 700,000, wakiwemo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Benezeth Lutenga Malinda, amesema mradi huo utaimarisha mifumo ya afya ya mifugo, maabara na ufuatiliaji wa magonjwa kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa maziwa, usalama wa chakula na kipato cha wafugaji nchini.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports