ELIMU YA USHINDANI NA ULINZI WA MLAJI KUANZA KUTOLEWA MASHULENI – Habari Mpya

Tume ya Ushindani (FCC) imesema imeanza mpango wa kuanzisha klabu za elimu ya ushindani, ulinzi wa mlaji na udhibiti wa bidhaa bandia katika shule za msingi, sekondari na taasisi za elimu ya juu ili kujenga kizazi chenye uelewa wa masuala hayo. Akizungumza na waandishi wa habari Juni 20, 2026, katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

Tume ya Ushindani (FCC) imesema imeanza mpango wa kuanzisha klabu za elimu ya ushindani, ulinzi wa mlaji na udhibiti wa bidhaa bandia katika shule za msingi, sekondari na taasisi za elimu ya juu ili kujenga kizazi chenye uelewa wa masuala hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari Juni 20, 2026, katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dodoma, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa FCC, Bi. Roberta Feruzi, amesema mpango huo utatekelezwa kupitia klabu zitakazojulikana kama Ushindani School Club. 

Amesema lengo la mpango huo ni kuwafikia wanafunzi mapema na kuwajengea uelewa kuhusu ushindani, haki za mlaji na namna ya kufanya maamuzi sahihi wanaponunua bidhaa au kupata huduma.

Feruzi amesema elimu hiyo itawasaidia wananchi kutambua bidhaa bandia, kulinda soko dhidi ya udanganyifu na kuwawezesha watumiaji kuchagua bidhaa salama na zenye ubora.

Ameeleza kuwa uelewa wa masuala ya ushindani na ulinzi wa mlaji utasaidia wananchi kufanya uchaguzi bora wa bidhaa na huduma, huku sekta binafsi ikiendelea kuchangia katika uzalishaji na ukuaji wa uchumi.

Aidha, amesema utoaji wa elimu hiyo utaendelea kupitia ofisi za kanda za FCC zilizopo Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma na Dar es Salaam kwa lengo la kuhakikisha wananchi katika mikoa yote ya Tanzania Bara wanapata elimu hiyo.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports