MKOMI AWATAKA WAKUU WA RASILIMALIWATU KUSHIRIKI KIKAO KAZI DODOMA – Habari Mpya

Na. Meleka Kulwa-Fullshangwe Blog,Dodoma ‎Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR-MUUUB), Bw. Juma Mkomi, amewataka Wakurugenzi na Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika taasisi za Serikali kushiriki kikao kazi kitakachofanyika Jijini Dodoma kuanzia Juni 1 hadi 3, 2026 kwa lengo la kujadili maboresho…

admin Avatar

by

2 minutes

Read Time

Na. Meleka Kulwa-Fullshangwe Blog,Dodoma

‎Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR-MUUUB), Bw. Juma Mkomi, amewataka Wakurugenzi na Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika taasisi za Serikali kushiriki kikao kazi kitakachofanyika Jijini Dodoma kuanzia Juni 1 hadi 3, 2026 kwa lengo la kujadili maboresho ya usimamizi wa rasilimaliwatu katika utumishi wa umma.

‎Ameyasema hayo Mei 26,2026 Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari , Aidha, Mkomi amesema kikao hicho kitawakutanisha viongozi kutoka Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

‎Amesema kikao hicho kitaongozwa na kaulimbiu isemayo “Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Ulio Sikivu, Jumuishi, wenye Matokeo na Uwajibikaji Kuelekea Dira 2050.”

‎Aidha, Mkomi amebainisha kuwa kikao kazi hicho hufanyika kila mwaka kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kuimarisha ufanisi wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali katika usimamizi wa rasilimaliwatu.

‎Ameongeza kuwa kikao hicho kitajadili matumizi ya mifumo mbalimbali ya kidijitali ikiwemo e-Uhamisho, e-Watumishi, e-Utendaji, e-Mrejesho pamoja na HR Assessment kwa kuzingatia vipaumbele vya Taifa kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

‎Pia amesema washiriki watapata nafasi ya kujadili mafanikio na changamoto zilizopo katika Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu pamoja na kupendekeza njia bora za kukabiliana nazo.

‎Katika hatua nyingine, Mkomi amesisitiza viongozi wote wenye dhamana ya kusimamia rasilimaliwatu kushiriki kikao hicho wao wenyewe bila ya kuwakilishwa kutokana na umuhimu wake.

‎Amebainisha kuwa mgeni rasmi katika kikao hicho anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani  Kikwete.

‎Sambamba na hilo, Mkomi amesema washiriki wote wanatakiwa kujisajili kupitia mfumo wa TSMS kwa kutumia tovuti ya [TSMS](https://tsms.gov.go.tz kabla ya Mei 29, 2026 saa 6:00 usiku ili kurahisisha maandalizi ya kikao hicho.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports