WAZIRI MKUU ATETA NA RAIS WA BENKI YA AfDB – Habari Mpya

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Sidi Ould Tah kando ya Mkutano wa 61 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika unaofanyika leo Jumanne Mei 26, 2026 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kintele (Kintele Congress Centre) jijini…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Sidi Ould Tah kando ya Mkutano wa 61 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika unaofanyika leo Jumanne Mei 26, 2026 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kintele (Kintele Congress Centre) jijini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo.

Mazungumzo hayo yalijikita katika masuala mbalimbali ya maendeleo pamoja na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na taasisi hiyo.

Dkt. Mwigulu anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo unaowakutanisha viongozi mbalimbali wa Afrika pamoja na wadau wa maendeleo kujadili masuala ya uchumi, uwekezaji na maendeleo ya bara la Afrika.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports