TANZANIA YAREJESHA USHIRIKIANO WA KIDIPLOMASIA NA HUNGARY BAADA YA MIAKA 35 – Habari Mpya

Na. Fullshangwe Blog,Bungeni Dodoma ‎Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amesema kuwa Tanzania na Hungary zimefungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kidiplomasia baada ya Hungary kufungua tena ubalozi wake jijini Dar es Salaam baada ya zaidi ya miaka 35. ‎Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

Na. Fullshangwe Blog,Bungeni Dodoma

‎Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amesema kuwa Tanzania na Hungary zimefungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kidiplomasia baada ya Hungary kufungua tena ubalozi wake jijini Dar es Salaam baada ya zaidi ya miaka 35.

‎Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Leo Mei 26,3026 bungeni jijini Dodoma, Mhe. Kombo amesema kuwa hatua hiyo ilifikiwa kufuatia ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary nchini Tanzania mwezi Septemba 2025.

‎Aidha, amebainisha kuwa nchi hizo mbili zilisaini Hati ya Makubaliano kati ya Kituo cha Kidijitali Tanzania na Kampuni ya MeOut kuhusu masuala ya ubunifu na teknolojia.

‎Pia ameongeza kuwa kurejea kwa ubalozi huo kunaonesha kuongezeka kwa imani ya kimataifa kwa Tanzania pamoja na kufungua fursa mpya za biashara, uwekezaji na ushirikiano wa kiteknolojia.

‎Kombo amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha uhusiano wa kimataifa kwa manufaa ya maendeleo ya taifa.

‎Katika mwaka wa fedha 2026/2027, Wizara imeomba kuidhinishiwa zaidi ya shilingi bilioni 353 kwa ajili ya shughuli zake.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports