UONGOZI WA TAGCO MGUU SAWA MAANDALIZI YA TAGCO AGM 2026 – Habari Mpya

Uongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) ukiongozwa na Mwenyekiti wake Bw. Karimu Meshack umewasili jijini Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano mkuu wa Mwaka wa TAGCO unaotarajiwa kufanyika Jijini Mwanza kuanzia tarehe 1-5 Juni, 2026. Ukiwa Jijini Mwanza uongozi huo umemtembelea mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda kwa lengo…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

Uongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) ukiongozwa na Mwenyekiti wake Bw. Karimu Meshack umewasili jijini Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano mkuu wa Mwaka wa TAGCO unaotarajiwa kufanyika Jijini Mwanza kuanzia tarehe 1-5 Juni, 2026.

Ukiwa Jijini Mwanza uongozi huo umemtembelea mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda kwa lengo la kujitambulisha na kumuelezea ratiba ya mkutano huo ambapo maafisa Mwasiliano wa Serikali watapata wasaa wa kubadilishana uzoefu, mbinu mbalimbali za kuimarisha utendaji kazi, mafunzo, kuhamasisha shughuli za kijamii, kushiriki michezo na kuhamasisha utalii wa ndani ambapo zaidi ya wanachama 500 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports