MZEE KAYUMBA AIPONGEZA VETA, ASISITIZA MATUMIZI YA BIDHAA NA UJUZI WA NDANI – Habari Mpya

Na Meleka Kulwa-Fullshangwe Blog, Dodoma Mzee Kayumba, mkazi wa Dodoma, amefurahishwa na huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) pamoja na bidhaa zinazotengenezwa na mamlaka hiyo, akibainisha kuwa vijana wa Kitanzania wanafanya kazi kubwa yenye ubora unaovutia. Amesema hayo Juni 19, 2026 alipotembelea banda la VETA katika Maadhimisho ya Wiki…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

Na Meleka Kulwa-Fullshangwe Blog, Dodoma

Mzee Kayumba, mkazi wa Dodoma, amefurahishwa na huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) pamoja na bidhaa zinazotengenezwa na mamlaka hiyo, akibainisha kuwa vijana wa Kitanzania wanafanya kazi kubwa yenye ubora unaovutia.

Amesema hayo Juni 19, 2026 alipotembelea banda la VETA katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

Amebainisha kuwa amefurahishwa na vifaa vinavyotengenezwa na VETA, akisema vinaonyesha ubunifu mkubwa wa vijana wa Kitanzania na kwamba vinapendeza.

Aidha, amesema kuwa VETA inapaswa kuendelea kuwajengea uwezo vijana katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali, akibainisha kuwa maendeleo ya nchi yanaweza kupatikana kwa kutumia bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi.

Pia ameongeza kuwa bidhaa zinazotengenezwa na vijana wa Kitanzania ni bora, na kwamba Watanzania wanapaswa kuzithamini na kuzitumia.

Aidha, ametoa wito kwa vijana na wazazi kutembelea mabanda ya VETA ili kujifunza fursa zilizopo, huku akiwahimiza vijana kujiunga na vyuo vya ufundi ili kupata ujuzi utakaowawezesha kujiajiri na kuajiri wengine.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports