RC Mara aingilia kati sakata la fedha za upimaji ardhi Rorya

Rorya. Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani humo kushirikiana na Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) kuchukua hatua za kiutawala dhidi ya watumishi wa idara ya ardhi wanaodaiwa kusababisha hasara ya zaidi ya Sh108 milioni. Fedha hizo zilitolewa katika mwaka wa fedha…

admin Avatar

by

2 minutes

Read Time

Rorya. Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani humo kushirikiana na Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) kuchukua hatua za kiutawala dhidi ya watumishi wa idara ya ardhi wanaodaiwa kusababisha hasara ya zaidi ya Sh108 milioni.

Fedha hizo zilitolewa katika mwaka wa fedha 2022/23 kwa ajili ya upimaji, upangaji na urasimishaji wa ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, lakini kazi hiyo haikukamilika licha ya wapima ardhi hao kudaiwa kupokea malipo hayo.

Mtambi ametoa agizo hilo Juni 18, 2026 katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya kilichojadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Amesema uchunguzi wa Takukuru kuhusu suala hilo umekamilika na majalada yamewasilishwa kwa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka, hivyo hatua za kiutawala zinaweza kuendelea sambamba na mchakato wa kisheria.

“Takukuru wamesema tayari uchunguzi umekamilika na majalada ya wahusika yamepelekwa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka. Niiombe Takukuru kwa kushirikiana na RAS muone namna ya kuwawajibisha kiutawala, kama inawezekana kiasi hiki cha fedha kikatwe kwenye mishahara yao ili kirudishwe halmashauri,” amesema Mtambi.

Amesema fedha hizo ni muhimu kwa halmashauri hiyo kwani upimaji na urasimishaji wa ardhi ungewezesha uuzaji wa viwanja na kuongeza mapato ya ndani.

Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Rorya wakiwa kwenye kikao maalum cha kujibu hoja za ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2024/25. Picha na Beldina Nyakeke

Mtambi ametoa siku saba kwa Ofisa Ardhi wa halmashauri hiyo kuwasilisha taarifa kamili inayoonesha ukubwa wa eneo lililotakiwa kupimwa, kiasi kilichopimwa na hatua zilizofikiwa na wapima ardhi hao.

“Mmesema hawa wapima ardhi walichukua fedha na kuondoka bila kukamilisha kazi. Nataka taarifa inayoeleza walitakiwa kupima ekari ngapi na wao walipima kiasi gani. Hili jambo ni lazima tulimalize,” amesema.

Aidha, amelitaka Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Rorya kuisimamia menejimenti ya halmashauri hiyo kwa karibu ili kuhakikisha majukumu yanatekelezwa kwa ufanisi na wananchi wanapata huduma bora.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Abdul Mtaka, amesema halmashauri imeshindwa kuuza viwanja hivyo kutokana na upimaji kutokamilika kama ilivyopangwa.

Amesema tayari wamewasiliana na Kamishna wa Ardhi wa Mkoa kuhusu suala hilo ili kupata mwelekeo wa hatua za kuchukua dhidi ya wapima ardhi hao.

“Viwanja hivyo vilitarajiwa kuuzwa kwa wananchi na kusaidia halmashauri kuongeza mapato ya ndani,” amesema.

Naye Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Juma Oketho, amesema halmashauri imepokea zaidi ya Sh3.5 bilioni kutoka Serikali Kuu tangu Desemba 2025 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo elimu, afya na utawala.

Amesema pia halmashauri imeboresha ukusanyaji wa mapato na kufikia zaidi ya asilimia 107 ya malengo yaliyowekwa.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports