Serikali yasifu ujenzi wa sekondari Bahi

DODOMA: Serikali imeipongeza Benki ya NMB kwa kujenga Shule ya Sekondari ya Bweni kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wilayani Bahi mkoani Dodoma. Mradi uliogharimu Sh bilioni 5 na kukamilika kwa asilimia 100. Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu, Atupele Mwambene, amesema shule hiyo imejengwa kwa kiwango cha juu na ina mabweni, vitanda, madawati pamoja na uwezo…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

DODOMA: Serikali imeipongeza Benki ya NMB kwa kujenga Shule ya Sekondari ya Bweni kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wilayani Bahi mkoani Dodoma. Mradi uliogharimu Sh bilioni 5 na kukamilika kwa asilimia 100.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu, Atupele Mwambene, amesema shule hiyo imejengwa kwa kiwango cha juu na ina mabweni, vitanda, madawati pamoja na uwezo wa kuhudumia wanafunzi 160. Inatarajiwa kuanza kupokea wanafunzi Januari 2027 baada ya usajili.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bahi, Albina Mtumbuka, amesema halmashauri iko tayari kuipokea na kuitunza shule hiyo, huku akiwataka wazazi kutowaficha watoto wenye mahitaji maalumu.

Mkurugenzi wa Uhusiano na Wawekezaji, Uendelevu na Mawasiliano wa NMB, Innocent Yonazi, amesema mradi huo unalenga kupanua fursa za elimu kwa watoto wenye mahitaji maalumu. NMB imetoa zaidi ya Sh bilioni 24 kwa miradi ya kijamii katika miaka mitano.

 

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports