Raia wa China akamatwa kwa kuwashambulia wafanyakazi Morogoro

Morogoro. Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia raia wa China anayefanya kazi katika Kampuni ya TBEA, kwa tuhuma za kuwashambulia wafanyakazi wenzake wawili katika Wilaya ya Mvomero, huku likiendelea kumtafuta mshukiwa mwingine anayedaiwa kushiriki katika tukio hilo. Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 20, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

Morogoro. Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia raia wa China anayefanya kazi katika Kampuni ya TBEA, kwa tuhuma za kuwashambulia wafanyakazi wenzake wawili katika Wilaya ya Mvomero, huku likiendelea kumtafuta mshukiwa mwingine anayedaiwa kushiriki katika tukio hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 20, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Endrew Kantimbo amesema mtuhumiwa anayeshikliwa ni Zhou Zhi (36), fundi minara katika Kampuni ya TBEA.

Amesema tukio hilo lilitokea Juni 19, 2026 katika Kitongoji cha Sokoine Ranch, Kijiji cha Wami Sokoine, Kata ya Dakawa, Wilaya ya Mvomero, ambapo Zhou Zhi akishirikiana na raia mwenzake wa China anayefahamika kwa jina la Yung Lu, waliwashambulia wafanyakazi hao kwa kutumia kitu butu.

Waliojeruhiwa ni Stephen Mwampaka (44), dereva wa Kampuni ya TBEA, pamoja na Mbaraka Ally (18), ambaye ni kibarua katika kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa Kamanda Kantimbo, waathirika hao walipata majeraha katika sehemu mbalimbali za miili yao na walipatiwa matibabu na chanzo cha tukio hilo kinaendelea kuchunguzwa na Jeshi la Polisi.

Amesema mtuhumiwa Zhou Zhi anaendelea kushikiliwa katika Kituo cha Polisi Mvomero kwa ajili ya mahojiano na hatua nyingine za kisheria, huku juhudi za kumkamata Yung Lu zikiendelea.

Katika tukio jingine, Jeshi la Polisi linawashikilia Fadhili Nyambalo (19) pamoja na watuhumiwa wengine kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa pikipiki tatu aina ya Haojue na uporaji wa simu za mkononi, yaliyotokea katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Mvomero kati ya Mei 21 na Mei 28, 2026.

Kamanda Kantimbo amesema matukio hayo yalitokea katika Kitongoji cha Kingurungunda, Kijiji cha Mbigiri na Kitongoji cha Sokoine Ranch, Kijiji cha Wami Sokoine, Kata ya Dakawa, ambapo watuhumiwa wanadaiwa kutekeleza vitendo vya uporaji na wizi.

Amesema uchunguzi wa matukio yote unaendelea na watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports