NIMEFANYA ZIARA KATIKA NCHI ILIYOWEKA ALAMA KWA TAIFA LA NAMIBIA, RAIS NANDI-NDAITWAH  – Habari Mpya

Rais wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah Juni 21, 2026 amefanya ziara katika Kambi ya Kihistoria ya Wapigania Uhuru wa nchi yake iliyopo Kongwa mkoani Dodoma.  Rais Nandi-Ndaitwah amesindikizwa na viongozi waandamizi wa Serikali wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Prof. Palamagamba Kabudi kutembelea kambi hiyo liyobeba…

admin Avatar

by

2 minutes

Read Time

Rais wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah Juni 21, 2026 amefanya ziara katika Kambi ya Kihistoria ya Wapigania Uhuru wa nchi yake iliyopo Kongwa mkoani Dodoma.

 Rais Nandi-Ndaitwah amesindikizwa na viongozi waandamizi wa Serikali wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Prof. Palamagamba Kabudi kutembelea kambi hiyo liyobeba uzito mkubwa wa uhusiano wa kihistoria na kidiplomasia kwa mataifa hayo mawili. 

Akiwa kwenye kambi hiyo, Rais Nandi-Ndaitwah alioneshwa majengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Bweni alilowahi kuishi Rais wa kwanza wa Namibia, Hayati Sam Nujoma, madarasa ya mafunzo ya wapigania uhuru, mahandaki, maeneo ya kulenga shabaha na makaburi waliozikwa wapigania uhuru.

Kwenye makaburi hayo Mhe. Nandi-Ndaitwah alitoa heshima za nwisho kwenye makaburi matatu waliozikwa wapigania uhuru wa Chama cha Ukombozi cha SWAPO. Kwenye kambi hiyo kuna makaburi 12 waliozikwa wapigania uhuru, yakiwemo matatu ya wanachama wa ANC na 5 yaliyosalia wamezikwa wapigania uhuru wa FRELIMO.

Baada ya kutoa heshima za mwisho, Rais Nandi-Ndaitwah aliongea na wanachi wa Kongwa na kuelezea shukrani zake za dhati kwa Tanzania kutokana na mchango mkubwa wa damu na mali kwa nchi za Afrika ikiwemo Namibia.

Alieleza wapigania uhuru wa nchi zote wameishi Tanzania akiwemo mume wake ambaye alikuwa mmoja wa waliopata mafunzo kwenye kambi ya Kongwa.

Aliongeza kuwa anauthamini mchango wa Tanzania ndiyo maana alimwalika Rais Samia Suluhu Hassan kama Mgeni Maalum wakati wa uapisho wake na kufanya ziara ya kujitambulisha nchini Tanzania mwezi Mei 2025. “Nimesema nije tena kufanya ziara ya kitaifa kwa nchi ambayo imeweka alama kwa Taifa la Namibia”, Alisema Rais Nandi-Ndaitwah.

Rais Nandi-Ndaitwah kabla ya kurejea jijini Dar Es Salaam alipata fursa ya kutembelea kiwanja kilichotolewa na Serikali bure katika Mji wa Serikali kwa ajili ya ujenzi wa ubalozi na kuahidi kuwa hivi karibuni Serikali itafanya jambo kwenye kiwanja hicho.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports