TANZANIA NA MAREKANI ZAENDELEZA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI KATIKA SEKTA MUHIMU – Habari Mpya

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Ellen Maduhu, amefanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Mhe. Andrew Lentz, kuhusu kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Marekani. Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walijadili namna ya kuendeleza na kuimarisha…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Ellen Maduhu, amefanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Mhe. Andrew Lentz, kuhusu kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Marekani.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walijadili namna ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, huduma za kibalozi, biashara na uwekezaji, usalama, nishati pamoja na utekelezaji wa mipango ya kimkakati ya maendeleo.

Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Dkt. Elsie S. Kanza, ambaye alishiriki katika majadiliano yaliyolenga kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.

Aidha, pande zote mbili zilisisitiza dhamira yao ya kuendelea kushirikiana na kufanya mazungumzo yenye tija kwa manufaa ya mataifa hayo mawili.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports