Serikali yaja na mkakati mazingira kufikia uchumi wa kati na juu

Mbeya. Serikali imesema imeweka mkakati wa kuimarisha usimamizi wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kama nguzo muhimu ya kufikia uchumi wa kati na juu. Akizungumza leo Mei 24, 2026  jijini Mbeya wakati wa maandalizi ya Siku ya Mazingira Duniani, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dk Richard Muyungi amesema…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

Mbeya. Serikali imesema imeweka mkakati wa kuimarisha usimamizi wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kama nguzo muhimu ya kufikia uchumi wa kati na juu.

Akizungumza leo Mei 24, 2026  jijini Mbeya wakati wa maandalizi ya Siku ya Mazingira Duniani, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dk Richard Muyungi amesema Tanzania inalenga kuimarisha mazingira kama sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Maendeleo.

Amesema Tanzania inazalisha takribani tani milioni 17 hadi 20 za taka kwa mwaka, ambapo Serikali inalenga kuhakikisha asilimia 70 ya taka hizo zinabadilishwa kuwa malighafi zenye faida kupitia teknolojia na ubunifu wa vijana.

“Tunataka hizi taka ziwe mali. Vijana wetu wana uwezo wa kutumia teknolojia kubadili taka kuwa bidhaa zenye thamani,” amesema.

Ameongeza kuwa mabadiliko hayo yatasaidia kufikia lengo la kipato cha wastani cha dola 7,000 kwa kila Mtanzania katika miaka ijayo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Rodrick Mpogolo amesema mkoa umejipanga katika kampeni ya upandaji miti, ambapo lengo ni kupanda miti 1,500 kila mwaka na kufikia miti milioni 1.5 ndani ya miaka 10.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk Richard Muyungi akishirikiana na wananchi na baadhi ya viongozi mkoani Mbeya kufanya usafi katika stendi ya daladala Kabwe jijini Mbeya.

Amesema Mbeya ina fursa kubwa za kiutalii na mazingira mazuri yanayoweza kuifanya kuwa mfano wa Taifa katika uhifadhi wa mazingira.

Vijana wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), wamesema wako tayari kutumia ujuzi wao endapo watapatiwa sapoti ya kutosha ili kuchangia maendeleo ya taifa.

Wananchi pia wamepongeza maboresho ya usafi jijini Mbeya, wakisema hali ya mazingira imeimarika ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports