Wazazi walalamika kuchangishwa fedha kununua picha ya Rais, bendera ya Taifa

Hanang. Wananchi wa kijiji cha Mogitu, wilayani Hanang mkoani Manyara, wamelalamikia kitendo cha kuchangishwa fedha kwa ajili ya ununuzi wa picha ya Rais na bendera ya Taifa. Wakazi wa kijiji hicho wenye wanafunzi katika Shule Msingi Mogitu ambayo ni mpya wametakiwa kuchangia Sh3,200 kila mmoja ili zipatikane Sh400,000 za kununua picha ya Rais na bendera…

admin Avatar

by

2 minutes

Read Time

Hanang. Wananchi wa kijiji cha Mogitu, wilayani Hanang mkoani Manyara, wamelalamikia kitendo cha kuchangishwa fedha kwa ajili ya ununuzi wa picha ya Rais na bendera ya Taifa.

Wakazi wa kijiji hicho wenye wanafunzi katika Shule Msingi Mogitu ambayo ni mpya wametakiwa kuchangia Sh3,200 kila mmoja ili zipatikane Sh400,000 za kununua picha ya Rais na bendera ya Taifa vya kuwekwa kwenye ofisi ya mwalimu mkuu.

Wakitoa malalamiko yao Mei 23, 2026 kwenye ziara ya Mbunge wa Hanang (CCM), Asia Halamga   walilalamikia kuchangishwa fedha hizo.

Mmoja kati ya wakazi hao, James Hando alisema kila mwanafunzi anayesoma shule hiyo aliagizwa kuchangia Sh3,200 hivyo mzazi mwenye watoto watatu anapaswa kuchangia Sh9,600.

“Serikali imetoa fedha nyingi kwa kujenga madarasa, vyoo na ofisi ya shule, inakuwaje inashindwa kuwa na picha ya Rais kuweka katika ofisi ya mwalimu mkuu na bendera ya kupepea uwanjani au Serikali imeishiwa,” alihoji.

Mkazi mwingine wa kijiji hicho, Magreth Ombay alisikitishwa na kitendo hicho kwani hizo ni alama muhimu za Taifa ila hazipaswi kuchangiwa fedha na wanafunzi kupitia wazazi na walezi.

Ombay alisema huo ni wajibu wa viongozi wa shule kufuatilia na kutoa taarifa kwa ngazi za juu za maofisa elimu kata na wilaya na siyo kuchangishwa wanafunzi.

Akijibu kero hizo, Asia alisema picha ya Rais na bendera ya Taifa huwa haichangiwi ili kununuliwa.

“Hilo halipo suala la kuwachangisha wananchi wa kijiji ili wanunue bendera ya Taifa na picha ya Rais kwani huwa inapelekwa sehemu husika haichangiwi,” alisema.

Ofisa elimu wa kata ya Mogitu, John Aloyce alisema suala hilo halijafika ofisini kwake hivyo atalifuatilia ili kubaini msingi wa hatua hiyo.

“Suala hilo nalibeba nitafuatilia kwani ndiyo mara ya kwanza kulisikia hapa kuwa wananchi wameagizwa kuchangia hizo fedha,” alisema.

Diwani wa Mogitu, Ng’wani Baghari alisema shule hiyo ni mpya ila hakupata taarifa kuna utaratibu unaotumika wa kuchangishwa fedha kwa wazazi na walezi kupitia wanafunzi.

“Inapoanzisha shule aidha ya kitongoji kabla ya usajili inakuwa inahudumiwa na shule mama kama ya kijiji kwa walimu na vifaa vya ufundishaji vyote, pengine mzigo ukiwa mzito kwa shule mama ndiyo ile sasa walimu wanatafuta kwa wadau wengine ili shughuli ziende,” alisema Ng’wani.

Alisema shule hiyo ipo kando ya barabara kuu ya kwenda Singida ni ya kitongoji na ni mpya imeanza Januari mwaka 2026 kwa kuwamega wanafunzi wa shule mama ya Mogitu.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports