SERIKALI YAHAKIKISHA MAZINGIRA BORA KATIKA MAKAZI YA WATOTO NCHINI – Habari Mpya

Na Jackline Minja, Dodoma Serikali imeendelea kuweka utaratibu madhubuti wa kuhakikisha watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto wanakuwa katika mazingira bora, salama na yenye kuzingatia ustawi wao kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo ya nchi. Kauli hiyo imetolewa bungeni na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mhandisi…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

Na Jackline Minja, Dodoma

Serikali imeendelea kuweka utaratibu madhubuti wa kuhakikisha watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto wanakuwa katika mazingira bora, salama na yenye kuzingatia ustawi wao kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa bungeni na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Lucy Simirya Kombani, aliyetaka kujua Serikali imejipangaje kuhakikisha watoto wanaoishi kwenye vituo vya kulelea watoto wanaishi katika mazingira bora na salama.

Mahundi amesema Makao ya Watoto nchini yanaanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto Sura ya 13, Kanuni za Makao ya Watoto za mwaka 2012 pamoja na Mwongozo wa Taifa wa Uanzishaji, Uendeshaji na Usimamizi wa Makao ya Watoto wa mwaka 2024.

 “Utaratibu wa usajili wa makao hayo huanzia katika ngazi ya Kata na Halmashauri kabla ya kuwasilishwa Wizara husika kupitia Kamishna wa Ustawi wa Jamii kwa ajili ya kupata leseni ya usajili baada ya kukidhi vigezo vyote vilivyowekwa aidha Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka ngazi ya Wizara, Mkoa na Halmashauri wanaendelea kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa mara kwa mara katika makao hayo ili kuhakikisha watoto wanapatiwa huduma bora za malezi, ulinzi na usalama wakati wote”. Aliseme Mhe Mahundi

Serikali imeeleza kuwa hatua hizo ni sehemu ya dhamira ya kuhakikisha watoto wote wanaolelewa katika vituo mbalimbali wanapata haki zao za msingi na kukua katika mazingira yenye upendo, malezi bora na usalama.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports