TANZANIA NA VIETNAM KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI KATIKA ELIMU, BIASHARA NA MAENDELEO – Habari Mpya

Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australia Bi .Felista Rugambwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya kisoshalisti ya Vietnam Nchini Tanzania Bi Vu Thanh Huyen ,Juni 19 2026 Jijini Dodoma. Katika mazungumzo hayo, Bi Felista amesisitiza dhamira ya Tanzania kuendeleza na kuimarisha ushirikiano na Vietnam hususani katika sekta ya elimu ya juu. …

admin Avatar

by

2 minutes

Read Time

Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australia Bi .Felista Rugambwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya kisoshalisti ya Vietnam Nchini Tanzania Bi Vu Thanh Huyen ,Juni 19 2026 Jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, Bi Felista amesisitiza dhamira ya Tanzania kuendeleza na kuimarisha ushirikiano na Vietnam hususani katika sekta ya elimu ya juu. 

Amesema Tanzania inathamini mchango wa ushirikiano wa kimataifa katika kukuza rasilimali watu, utafiti na ubunifu, na kwamba hatua ya kuunganisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na vyuo vikuu vya Vietnam itakuwa chachu muhimu ya maendeleo ya elimu na teknolojia kati ya mataifa hayo mawili.

Kwa upande wake, Balozi Vu Thanh Huyen ameishukuru Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuwezesha upatikanaji wa kiwanja katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba, akieleza kuwa hatua hiyo ni ishara muhimu ya kuimarika kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Vietnam.

Aidha, Balozi Huyen ameonesha utayari wa Vietnam wa kuendeleza ushirikiano katika sekta ya elimu ya juu, ambapo amesema yupo tayari kusaidia kuimarisha ushirikiano wa kitaaluma kati ya Tanzania na Vietnam.

Vilevile, pande zote mbili zimejadili maandalizi ya Mkutano wa Pili wa Tume ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Vietnam, unaotarajiwa kufanyika Septemba 2026. Mkutano huo unatarajiwa kuimarisha zaidi ushirikiano katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, mawasiliano, biashara na uwekezaji, pamoja na kuongeza fursa mpya za kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.

Katika hatua nyingine, Balozi Huyen ameahidi kufuatilia kwa karibu rasimu za mikataba na hati za makubaliano zilizowasilishwa Vietnam ili kupata mrejesho wake, hatua itakayosaidia kuimarisha utekelezaji wa makubaliano katika sekta za elimu, umwagiliaji, teknolojia na ushirikiano wa kidiplomasia.

Mazungumzo hayo yanaonesha dhamira ya pamoja ya kuimarisha uhusiano na Ushrikiano kati ya Tanzania na Vietnam kwa manufaa ya pande zote mbili.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports