Absa, TPSF wawajengea uwezo wanawake wajasiriamali

Dar es Salaam. Benki ya Absa Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), imeendesha semina maalumu kwa wanawake wajasiriamali wadogo na wa kati kutoka sekta mbalimbali kwa lengo la kuwajengea uwezo katika masuala ya elimu ya fedha, uwekezaji na usimamizi wa biashara. Semina hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki,…

admin Avatar

by

3 minutes

Read Time

Dar es Salaam. Benki ya Absa Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), imeendesha semina maalumu kwa wanawake wajasiriamali wadogo na wa kati kutoka sekta mbalimbali kwa lengo la kuwajengea uwezo katika masuala ya elimu ya fedha, uwekezaji na usimamizi wa biashara.

Semina hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, imewakutanisha wanawake kutoka maeneo mbalimbali nchini ili kupata maarifa yatakayowasaidia kufanya uamuzi sahihi wa kifedha na kuimarisha shughuli zao za kiuchumi.

Akizungumza wakati wa semina hiyo, Meneja wa Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Abigail Lukuvi amesema mpango huo ni sehemu ya ajenda ya uwajibikaji kwa jamii ya benki hiyo, inayolenga kuwawezesha wananchi, hususan wanawake wajasiriamali, kupata elimu ya kifedha itakayowawezesha kukuza biashara zao na kuongeza mchango wao katika maendeleo ya uchumi.

Amesema Absa inaamini kuwa kuwawezesha wanawake kupitia elimu na maarifa ya kifedha, ni hatua muhimu katika kujenga msingi imara wa mafanikio ya biashara zao na ustawi wa jamii kwa jumla.

Meneja wa Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Abigail Lukuvi akizungumza katika semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa  kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa wanawake wajasiriamali wadogo na wa kati ikihusu   elimu ya fedha na  usimamizi wa uwekezaji, jijini Dar es Salaam.

“Tunafurahi kuona mwitikio mkubwa wa wanawake katika mafunzo haya. Elimu wanayoipata itawasaidia kuimarisha biashara zao na kufikia malengo yao ya kiuchumi. Hii inaendana na dhamira ya Benki ya Absa ya kuchangia maendeleo ya Afrika kwa kuwawezesha watu na biashara kukua hatua kwa hatua,” amesema Lukuvi.

Ameongeza kuwa kupitia ushirikiano huo na TPSF, benki hiyo inaendelea kuwapa wanawake fursa ya kupata maarifa muhimu yatakayowasaidia kuboresha usimamizi wa fedha, uwekezaji na mipango ya ukuaji wa biashara zao.

Mkurugenzi wa Wanachama wa TPSF, Kinanasy Seif amesema taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuwawezesha wanawake wajasiriamali kupitia programu za mafunzo zinazolenga kukuza biashara na kuimarisha uchumi wao.

Amesema wanawake wana mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta binafsi na uchumi wa Taifa, hivyo ni muhimu kuendelea kuwajengea uwezo ili waweze kutumia kikamilifu fursa zilizopo katika mazingira ya biashara.

Meneja wa Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Abigail Lukuvi akizungumza katika semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa  kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa wanawake wajasiriamali wadogo na wa kati ikihusu   elimu ya fedha na  usimamizi wa uwekezaji, jijini Dar es Salaam.

“Tumefanikiwa kuwakutanisha wanawake wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali ili wapate elimu ya fedha na uwekezaji. Tunaamini maarifa haya yatawasaidia kufanya maamuzi bora ya kibiashara na kuongeza ushindani wa biashara zao,” amesema Kinanasy.

Katika semina hiyo, washiriki pia wamepata elimu kuhusu masuala ya kodi kutoka kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Ofisa Elimu kwa Mlipa Kodi na Mawasiliano kutoka Mkoa wa Kodi wa Kinondoni, Zephania Mange amesisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kuzingatia sheria za kodi ili kujenga biashara imara na endelevu.

Amesema walipakodi wana haki mbalimbali, ikiwamo kuhakikishiwa usiri wa taarifa zao za kikodi, kupata huduma kwa usawa na kupinga uamuzi wa kodi kwa kufuata taratibu zilizowekwa pale wanapoona hawajaridhika nayo.

Aidha, amewataka wafanyabiashara kujisajili kupata namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa wakati na kutekeleza wajibu wao wa kikodi kwa mujibu wa sheria ili kuchangia maendeleo ya Taifa na kuimarisha mazingira ya biashara nchini.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports