JESHI LA POLISI WAKUTANA NA MAWAKALA WA MABASI KUJADILI MIKAKATI YA USAFIRI SALAMA – Habari Mpya

Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani mkoani Arusha limeendelea kuimarisha mikakati ya kuzuia ajali za barabarani kwa kukutana na mawakala wa mabasi wanaotoa huduma za usafiri wa abiria ndani na nje ya Mkoa huo. Akizungumza mara baada ya kikao hicho leo, Mkuu wa Kikosi hicho Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Zauda…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani mkoani Arusha limeendelea kuimarisha mikakati ya kuzuia ajali za barabarani kwa kukutana na mawakala wa mabasi wanaotoa huduma za usafiri wa abiria ndani na nje ya Mkoa huo.

Akizungumza mara baada ya kikao hicho leo, Mkuu wa Kikosi hicho Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Zauda Mohamed amesema wamekutana na mawakala hao kuhakikisha sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani zinazingatiwa wakati wote.

ACP Zauda amebainisha kuwa kutokana na uwepo wa vituo vya mabasi maeneo mbalimbali mkoani humo, kupitia kikao hicho wameweka mpangokazi mzuri wa kukagua mabasi hayo pamoja na madereva kabla ya kuanza safari.

Pia amesema amesema kuwa ushirikiano wa karibu baina yao na wakala wa mabasi utasaidia kuondoa changamoto zinazowakabili abiria kwa wakati, huku lengo kuu likiwa ni kuhakikisha huduma ya usafiri inatolewa kwa kuzingatia usalama.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala Mabasi Mkoa wa Arusha (CMM) Bw. James Leonard amesema wataendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na kutoa taarifa muhimu zitakazosaidia kuimarisha usalama barabarani.

Aidha, ametoa wito kwa mawakala wenzake kuhakikisha mabasi yote, kabla ya kuanza safari yanakuwa katika hali nzuri kiufundi na kuendeshwa na madereva wenye weledi ili kuhakikisha usalama wa abiria na safari zenye utulivu wakati wote.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports