Sheria ya makisio na matumizi ya Sh8.5 trilioni yapitishwa Barazani

Unguja. Baraza la Wawakilishi Zanzibar, limepitisha Sheria ya Makisio na matumizi ya Sh8.5 trilioni kwa matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 31, 2027. Hatua hiyo ni kuruhusu utoaji na uhaulishaji wa fedha hizo pamoja na mambo mengine yanayohusiana na hayo. Sheria hiyo imepitishwa leo Juni 19, 2026 barazani hapo baada ya jana…

admin Avatar

by

3 minutes

Read Time

Unguja. Baraza la Wawakilishi Zanzibar, limepitisha Sheria ya Makisio na matumizi ya Sh8.5 trilioni kwa matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 31, 2027.

Hatua hiyo ni kuruhusu utoaji na uhaulishaji wa fedha hizo pamoja na mambo mengine yanayohusiana na hayo.

Sheria hiyo imepitishwa leo Juni 19, 2026 barazani hapo baada ya jana Juni 18, 2026 kumalizika mjadala na kupitishwa bajeti kuu ya Serikali mwaka 2026/27.

Awali, akitoa hoja kwa wajumbe wa baraza hilo, Waziri wa Fedha na Mipango,  Dk Juma Malik Akil aliwaomba wauzingatie na kujadili iwe sheria kwa matumizi ya Serikali.

Hata hivyo, ni mjumbe mmoja tu wa Pangawe, Ali Suleiman Ameir (CCM) aliyechangia muswada huo ambaye naye pia hakuwa na maeneo mengi ya kuchangia badala yake alitaka marekebisho tu ya kisarufi katika maeneo mawili.

Eneo mojawapo alitaka kuwemo na neno madhumuni ya sheria hiyo liandikwe kwani halijaandikwa kama inavyotakiwa na taratibu za kibajeti chini ya kanuni ya 84 na kifungu cha sita.

Waziri Malik amesema sheria hiyo ina vifungu vinane ambavyo ni jina fupi, tafsiri, utoaji wa Sh8.5 trilioni kwa matumizi ya Serikali, uwezo wa waziri kukopa, uwezo wa wazi maombi ya ziada na marejesho ya mkopo  na riba.

Amevitaja vifungu vingine kuwa ni  kukubaliwa fedha zitakazopitishwa kwa matumizi ya kazi za kawaida na miradi ya maendeleo na kiasi cha fedha kutoka mashirika ya maendeleo.

Kiasi cha Sh8.5 trilioni kinatolewa kwa ajili ya matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2027, ambapo Sh8.1 trilioni zinatolewa kwa ajili ya matumizi ya Serikali Kuu, Sh25.9 bilioni zinatolewa kwa ajili ya matumizi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa na Sh336.310 bilioni zinatolewa kwa Taasisi za Serikali zinazojitegemea.

Sheria hiyo inampa Waziri anayehusika na fedha anaweza wakati wowote sio zaidi ya Juni 30, 2027, kukopa kiasi chochote cha fedha ndani au nje ya Zanzibar.

Hata hivyo, isipokuwa kwamba jumla ya kiwango kilichokopwa hakizidi kiwango kilichotolewa au kinachochukuliwa kuwa kimetolewa kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali chini ya masharti ya kifungu cha 3 cha Sheria hii.

Ukopaji chini ya kifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki utafanywa kwa njia ya mkopo, mkopo wa awali, mkopo wa hati fungani wa muda mfupi, mkopo wa hati fungani wa muda mrefu au kukopa ziada kupitia hesabu za benki au hati nyingine yoyote ya ukopaji kwa vigezo na masharti kama Waziri atakavyoona inafaa.

Waziri anaweza, bila ya kujali masharti ya sheria hii au sheria nyingine yoyote, kuidhinisha matumizi ya ziada katika fungu lolote lililoidhinishwa katika jedwali la Sheria hii.

Hilo litatokea endapo Waziri anayehusika na fedha amejiridhisha kuwa, kwa masilahi ya umma, ni muhimu, kutoa matumizi ya ziada kwa Wizara, Idara au taasisi ya Serikali ikiwa ni zaidi ya fedha zilizokubalika kwa matumizi yaliyokusudiwa au huduma ambazo fedha zake hazijaidhinishwa na kwamba kuchelewesha matumizi hayo kutasababisha madhara kwa maslahi ya umma.

Endapo maombi ya ziada yameidhinishwa chini ya kifungu hiki, Waziri, haraka iwezekanavyo, baada ya uidhinishaji huo, atawasilisha mbele ya Baraza la Wawakilishi taarifa ya uhamishaji wa makadirio ya matumizi au ziada kama hali itakavyokuwa kwa mujibu wa masharti ya kifungu 106 (2) cha Katiba ya Zanzibar 1984.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports