RAIS WA NAMIBIA ATEMBELEA MAJIRANI ZAKE WA ZAMANI MAGOMENI – Habari Mpya

Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah, ametemebelea eneo la magomeni katika nyumba aliyowahi kuishi wakati wa harakati za ukombozi wa Namibia kupitia chama cha SWAPO. Katika ziara hiyo ya kipekee iliyochanganya hisia za kumbukumbu na mshikamano wa kihistoria kati ya Tanzania na Namibia, Rais Nandi-Ndaitwah alipokelewa kwa furaha na majirani zake hao…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah, ametemebelea eneo la magomeni katika nyumba aliyowahi kuishi wakati wa harakati za ukombozi wa Namibia kupitia chama cha SWAPO.

Katika ziara hiyo ya kipekee iliyochanganya hisia za kumbukumbu na mshikamano wa kihistoria kati ya Tanzania na Namibia, Rais Nandi-Ndaitwah alipokelewa kwa furaha na majirani zake hao wa Magomeni, akiwemo mama Salehe na mtoto wa mama Salama ambao walimfahamu tangu alipokuwa akiishi eneo hilo akiwa mwakilishi wa harakati za ukombozi.

Akizungumza na wakazi hao, Rais huyo alitoa shukurani zake kwa Serikali na wananchi wa Tanzania kwa mchango wao mkubwa katika harakati za ukombozi wa Namibia, akisisitiza kuwa historia hiyo imejenga uhusiano imara na wa kudumu kati ya mataifa hayo mawili.

“Magomeni ni sehemu ya maisha yangu na historia ya taifa langu. Tanzania ilitupa hifadhi, upendo na nafasi ya kupigania uhuru wetu. Huu ni ushahidi wa urafiki wa kweli na mshikamano wa Afrika,” alisisitiza.

Baada ya mazungumzo hayo, Rais Nandi-Ndaitwah alitembea nyumba aliyowahi kuishi, akapata fursa ya kukumbuka maisha ya miaka hiyo ya mapambano, huku majirani hao wakishiriki kumbukumbu na furaha ya kukutana tena na kiongozi huyo akiwa amefika kuwasilimu katika nafasi yake mpya ya Urais.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports