WANANCHI WAHOJI UHALALI WA VIPIMO VYA BANDO NA DAKIKA ZA MAONGEZI – Habari Mpya

 DODOMA Wakazi wa Jiji la Dodoma wameiomba Serikali kupitia Wakala wa Vipimo (WMA) kuingilia kati na kusimamia ipasavyo matumizi sahihi ya vipimo vya vifurushi vya intaneti “bando” pamoja na muda wa maongezi wakidai kupoteza data zao kwa haraka na bila uwazi. Wananchi hao wametoa wito wa kuwepo kwa uwazi na ukomo sahihi wa muda wa…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

 DODOMA

Wakazi wa Jiji la Dodoma wameiomba Serikali kupitia Wakala wa Vipimo (WMA) kuingilia kati na kusimamia ipasavyo matumizi sahihi ya vipimo vya vifurushi vya intaneti “bando” pamoja na muda wa maongezi wakidai kupoteza data zao kwa haraka na bila uwazi.

Wananchi hao wametoa wito wa kuwepo kwa uwazi na ukomo sahihi wa muda wa matumizi ya data, wakisema ni haki yao kupata kile wanacholipia.

Baadhi ya wakazi waliozungumza jijini hapa wameeleza kusikitishwa na namna megabytes (MBs) au gigabytes (GBs) wanazonunua zinavyoisha kwa muda mfupi hata pale wanapokuwa hawatumii simu zao kikamilifu, jambo linaloashiria kasoro kwenye usahihi wa vipimo hivyo

Meneja wa Wakala wa vipimo mkoa wa Dodoma Said Ibrahim, anasema wakala umepokea maoni hayo ya wadau na kuongeza kuwa umeshaanza mchakato wa kusimamia uhakiki ikiwemo katika vifurushi vya intaneti (Bando) na muda wa maongezi.




About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports