RAIS WA NAMIBIA ATEMBELEA KIWANJA CHA UBALOZI WA NAMIBIA KATIKA MJI WA SERIKALI MTUMBA – Habari Mpya

Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah leo tarehe 21 Juni, 2026, ametembelea kiwanja cha Ubalozi wa Namibia kilichopo katika Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma. Akiwasili katika Mji huo, Mhe. Rais Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah alipokelewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mhe. Prof. Palamagamba…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah leo tarehe 21 Juni, 2026, ametembelea kiwanja cha Ubalozi wa Namibia kilichopo katika Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma.

Akiwasili katika Mji huo, Mhe. Rais Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah alipokelewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.

Wakati wa ziara hiyo Katika Mji wa Serikali, Rais Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah alipata maelezo kuhusu mpango kabambe wa Mji wa Serikali pamoja na historia fupi ya maendeleo ya mji huo, ambayo yalitolewa na viongozi na wataalamu wanaosimamia utekelezaji wa mradi huo.

Katika kuendeleza ushirikiano na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Namibia, Rais Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah amepanda mti katika kiwanja cha Ubalozi wa Namibia na kuupa jina la “UMOJA TREE”, ikiwa ni ishara ya urafiki, mshikamano na ushirikiano endelevu kati ya mataifa hayo mawili.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports