ZAIDI YA VIJANA 35,000 KUSHIRIKI TAMASHA LA TWEN’ZETU KWA YESU, DAR ES SALAAM – Habari Mpya

Naibu Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Wilbroad Mastai akizungumza na waandishi wa habari  leo, Juni 11, 2026, jijini Dar es Salaam, …………… NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM Zaidi ya vijana 35,000 kutoka maeneo mbalimbali nchini wanatarajiwa kushiriki Tamasha la Twen’zetu kwa Yesu litakalofanyika…

admin Avatar

by

2 minutes

Read Time

Naibu Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Wilbroad Mastai akizungumza na waandishi wa habari  leo, Juni 11, 2026, jijini Dar es Salaam,

……………

NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM

Zaidi ya vijana 35,000 kutoka maeneo mbalimbali nchini wanatarajiwa kushiriki Tamasha la Twen’zetu kwa Yesu litakalofanyika Juni 13, 2026, katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, jijini Dar es Salaam, likiwa na lengo la kuwajengea vijana mtazamo chanya utakaowasaidia kuishi maisha mema mbele za Mungu na jamii.

Akizungumza leo, Juni 11, 2026, jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Wilbroad Mastai, amesema kuwa tamasha la mwaka huu limebeba kaulimbiu isemayo “Be the Star”, yenye maana kwamba vijana wanaweza kuishi maisha ya maadili mema na kutoufuata ulimwengu; badala yake, ulimwengu uwafuate wao.

Mchungaji Mastai amewataka vijana wa dini zote kushiriki Tamasha la Twen’zetu kwa Yesu, ambalo linalenga kuwaunganisha watu wa imani na itikadi mbalimbali katika umoja.

Amesema tofauti za kiimani na kiitikadi zinapaswa kutumika kujenga taifa lenye misingi ya nidhamu, kujituma, uwajibikaji, uzalendo na uraia mwema.

“Pia katika tamasha hili kutakuwa na vijana kutoka nchini Botswana ambao tayari wamewasili kwa ajili ya kujifunza jinsi tunavyoandaa tamasha hili, ili nao wapate uzoefu wa namna wanavyoweza kufanya shughuli kama hii nchini kwao,” amesema Mchungaji Mastai.

Ameeleza kuwa hili ni Tamasha la 13 tangu lilipoanzishwa mwaka 2014, huku akibainisha kuwa waimbaji watakaokuwepo
katika tamasha la mwaka huu ni Rose Mhando, Boaz Danken, Agape Gospel Band, Neema Gospel Choir, Hyper Squad, kwaya za KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), pamoja na Praise Team KKKT Kibangu.

Tamasha hilo litafungwa rasmi na Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Alex Malasusa, ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Mnenaji mkuu atakuwa Askofu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Dar es Salaam, Jackson Sostenes.

Tamasha litaanza saa 12:00 asubuhi na kuendelea hadi saa 12:00 jioni

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports