WAZIRI PROF. MKUMBO ATAJA MAENEO MATANO YA KIPAUMBELE MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA WA MWAKA 2026/27 – Habari Mpya

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo amewasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2026/27 akisisitiza vipaumbele vitano vya utekelezaji wake. Akitaja vipaumbele hivyo, amesema mosi ni kuimarisha utawala bora, demokrasia, amani, na utulivu na pili ni kujenga uchumi imara, jumuishi na shindani na kipaumbele cha tatu ni, kuimarisha…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo amewasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2026/27 akisisitiza vipaumbele vitano vya utekelezaji wake.

Akitaja vipaumbele hivyo, amesema mosi ni kuimarisha utawala bora, demokrasia, amani, na utulivu na pili ni kujenga uchumi imara, jumuishi na shindani na kipaumbele cha tatu ni, kuimarisha uwezo wa watu na maendeleo ya jamii.

Akiendelea kufafanua vipambele hivyo, Mhe. Waziri amesema kipaumbele cha nne ni kuimarisha uhifadhi wa mazingira na ustahimilivu kwa mabadiliko ya tabianchi na cha tano kikiwa kusimamia utekelezaji wa vichocheo vya mageuzi ambavyo ni pamoja na nishati, miundombinu ya usafiri na usafirishaji, utafiti na maendeleo, na mageuzi ya kidigitali.

Prof Kitila amesesema utekelezaji wa vipaumbele hivyo ni hatua za kuyatekeleza malengo makuu ya Dira 2050, na vimezingatia Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2026/27 – 2030/31 wenye dhima ya “Mageuzi kwa ajili ya Ukuaji Jumuishi wa Uchumi na Uzalishaji Ajira” ambao ni wa kwanza katika utekelezaji wa Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Muda Mrefu 2026/27 – 2050/51.

Aidha katika kutekeleza maeneo ya vipaumbele hivyo, Serikali imepanga kuanza kutekeleza programu na miradi mbalimbali ikiwemo miradi shikizi 38 kati ya 51 iliyopo katika programu saba (7) za kielelezo zilizoainishwa katika Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano.


About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports