Yanga wakitaka lao usilete mdomo!

KIGOMA;YANGA wakitaka lao usilete mdomo! Pengine ndivyo unavyoweza kuzungumzia matokeo ya mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara kati ya Mashujaa ya Kigoma na Yanga ya Dar es Salaam uliomalizika muda mfuoi uliopita Uwanja wa lake Tanganyika, Kigoma na wenyeji kulala kwa mabao 0-2. Kutokana na matokeo hayo Yanga imezidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

KIGOMA;YANGA wakitaka lao usilete mdomo! Pengine ndivyo unavyoweza kuzungumzia matokeo ya mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara kati ya Mashujaa ya Kigoma na Yanga ya Dar es Salaam uliomalizika muda mfuoi uliopita Uwanja wa lake Tanganyika, Kigoma na wenyeji kulala kwa mabao 0-2.

Kutokana na matokeo hayo Yanga imezidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo yenye timu 16, ikifikisha pointi 63, mbele ya mtani wake Simba yenye pointi 58. Simba ipo nyuma mchezo mmoja na itashuka uwanjani kesho kuivaa Pamba Jiji.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Mudathir Yahya na Bakari Mwamnyeto, hivyo kuzima tambo za kocha wa Mashujaa, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, ambaye kabla ya mchezo alitoa kauli za kubeza wachezaji wa Yanga hasa wale wa kigeni.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports