UVCCM KILIMANJARO “VIJANA MSITUMIKE KUVUNJA AMANI” – Habari Mpya

VIJANA wameaswa kutokukubali kurubuniwa, kushawishiwa wala kutumika kwa namna yoyote ili kuhatarisha Amani mshikamano na umoja wa Taifa kwa maslahi binafsi ya watu au makundi yenye nia zisizo njema kwa nchi. Tamko hilo limetolewa leo na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, Ivan Moshi mara baada ya kumalizika kwa…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

VIJANA wameaswa kutokukubali kurubuniwa, kushawishiwa wala kutumika kwa namna yoyote ili kuhatarisha Amani mshikamano na umoja wa Taifa kwa maslahi binafsi ya watu au makundi yenye nia zisizo njema kwa nchi.

Tamko hilo limetolewa leo na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, Ivan Moshi mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Baraza la UVCCM mkoa wa Kilimanjaro kilichofanyika katika ukumbi wa CCM mkoa.

Akisoma tamko hilo, Moshi alisema kuwa, wanatambua athari kubwa zinazoweza kusababishwa na migogoro, vurugu na mipasuko ya kijamii katika Uchumi na ustawi wa wananchi na kutoa wito kwa vijana kuendelea kuzipuuza kauli, vitendo na propaganda zinazolenga kuleta taharuki, migawanyiko au kuvuruga amani.

“Baraza la UVCCM mkoa wa Kilimanjaro linawapongeza vijana wa Kilimanjaro na Tanzania kwa kuendelea kuonyesha uzalendo, uvumilivu, busara na mshikamano katika kuilinda amani na utulivu wa Taifa letu, tunatambua amani ndio msingi wa maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa” alisema Ivan.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports