Mradi wa VETA Kilolo kutoa fursa za ajira

IRINGA: KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Kenani Kihongosi amesema kukamilika kwa mradi wa Chuo mafunzo ya ufundi (VETA)unaotekelezwa Kilolo kutafungua fursa kubwa za ajira na kujikwamua kiuchumi kwa vijana wa eneo hilo. Kihongosi ameeleza hayo leo Juni 19,2026 alipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Chuo Cha…

admin Avatar

by

2 minutes

Read Time

IRINGA: KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Kenani Kihongosi amesema kukamilika kwa mradi wa Chuo mafunzo ya ufundi (VETA)unaotekelezwa Kilolo kutafungua fursa kubwa za ajira na kujikwamua kiuchumi kwa vijana wa eneo hilo.

Kihongosi ameeleza hayo leo Juni 19,2026 alipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Chuo Cha VETA Kilolo unaotekelezwa katika Kijiji cha Luhindo Kata ya Mtitu Kilolo mkoani Iringa.

Akizungumza baada ya kukagua mradi huo, Kihongosi amesema kituo hicho kitawawezesha vijana kupata mafunzo yatakayowajengea ujuzi wa kujiajiri na kuajirika katika sekta mbalimbali za uzalishaji.

“Kwa sababu kukamilika kwa mradi huu kutaleta fursa kubwa kwa vijana wetu wa Wilaya ya Kilolo kuweza kupata mafunzo hapa ambayo yatawasaidia katika masuala ya ajira, lakini pia halmashauri wataweza kuwatumia vijana hao katika shughuli mbalimbali,” amesema.

Ameongeza kuwa uwepo wa karakana tatu ndani ya mradi huo utasaidia utoaji wa mafunzo ya vitendo yatakayowawezesha vijana kupata kipato na kuchangia ukuaji wa uchumi wa familia zao pamoja na Taifa kwa ujumla.

Kihongosi amesema chama na Serikali vitaendelea kushirikiana kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa asilimia 100 ili wananchi wa Kilolo wanufaike kikamilifu na uwekezaji huo wa maendeleo.

Awali akisoma taarifa ya mradi huo Mdhibiti Ubora wa Shule, Altos Kinunda amesema mradi huo unatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh bilioni 1.6 hadi kukamilika kwake. Hadi sasa umepokea Sh milioni 777.4, ambapo Sh milioni 573.7 zimetumika na Sh milioni 203.7 zimebaki kwa ajili ya kuendeleza ujenzi.

Amesema awamu ya kwanza inahusisha ujenzi wa majengo tisa ikiwemo utawala, madarasa, karakana mbalimbali, nyumba ya mtumishi, jengo la mlinzi na jengo la umeme, umefikia asilimia 76 ya utekelezaji na ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi 240.

“Mradi huu unatarajiwa kuleta manufaa makubwa kwa wananchi wa Kilolo na Taifa kwa ujumla, ikiwemo kutoa ajira kwa vijana na kina mama wakati wa ujenzi, kuongeza uzoefu wa usimamizi wa miradi mikubwa kwa wataalamu wa halmashauri na kuimarisha ushirikiano,” ameeleza Kinunda.

 

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports