OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAWAITA WANANCHI WIKI YA UTUMISHI WA UMMA – Habari Mpya

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imewakaribisha wananchi kutembelea banda la ofisi katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma, kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni, 2026.  Akizungumza katika Maadhimisho hayo Wakili wa Serikali wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. George Ngerema amewakaribisha wananchi kutembelea katika…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imewakaribisha wananchi kutembelea banda la ofisi katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma, kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni, 2026. 

Akizungumza katika Maadhimisho hayo Wakili wa Serikali wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. George Ngerema amewakaribisha wananchi kutembelea katika banda la Ofisi ili waweze kupata uelewa wa kina kuhusu masuala ya kisheria, majukumu ya Ofisi, na jinsi inavyosimamia maslahi ya taifa.

“Tunawakaribisha wananchi waweze kutembelea kwa wingi kwenye banda letu kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali za kisheria tutatoa huduma hii kwa wiki nzima ni tunaitoa bure kabisa”. Amesema Bw. Ngerema

Aidha, Bw. Ngerema ameeleza kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inayatumia maadhimisho hayo katika kusogeza huduma za serikali karibu na wananchi.

Amesema kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inatoa huduma za Elimu ya Sheria, msaada wa kisheria, utatuzi wa migogoro na kushughulikia malalamiko .

Maadhmisho ya Wiki Utumishi wa Umma mwaka 2026 yanafanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Doodma, yameanza tarehe 16 na yataendelea hadi tarehe 23 Juni, 2026 yamebeba kauli mbiu isemayo “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu”.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports