Veta Kilolo yafikia asilimia 76, vijana wapata matumaini

Kilolo. Matumaini ya vijana wa Wilaya ya Kilolo kupata elimu ya ufundi stadi na fursa za kujiajiri yameongezeka baada ya ujenzi wa Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta) unaoendelea katika Kijiji cha Luhindo, Kata ya Mtitu, kufikia asilimia 76. Mradi huo, unaogharimu zaidi ya Sh1.6 bilioni na unatekelezwa katika Mkoa wa Iringa,…

admin Avatar

by

2 minutes

Read Time

Kilolo. Matumaini ya vijana wa Wilaya ya Kilolo kupata elimu ya ufundi stadi na fursa za kujiajiri yameongezeka baada ya ujenzi wa Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta) unaoendelea katika Kijiji cha Luhindo, Kata ya Mtitu, kufikia asilimia 76.

Mradi huo, unaogharimu zaidi ya Sh1.6 bilioni na unatekelezwa katika Mkoa wa Iringa, unatarajiwa kuwawezesha vijana kupata ujuzi unaohitajika katika soko la ajira na kujitegemea kiuchumi.

Hayo yameelezwa leo Juni 19, 2026 wakati wa ziara ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, aliyefika kukagua utekelezaji wa mradi huo unaosimamiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo.

Baada ya kukagua mradi huo, Kihongosi amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhakikisha miundombinu inayojengwa inalindwa ili kudumu na kuwanufaisha wananchi kwa muda mrefu.

Amesema elimu ya ufundi stadi ni moja ya nguzo muhimu za maendeleo ya Taifa kwa kuwa huwapa vijana maarifa na stadi zinazowawezesha kushiriki kikamilifu katika uzalishaji na ujenzi wa uchumi.

Kwa mujibu wa taarifa ya mradi iliyowasilishwa na Ofisa Udhibiti Ubora wa Shule Wilaya ya Kilolo, Alto Kinunda, chuo hicho kinajengwa katika eneo lenye ukubwa wa ekari 38.16 na utekelezaji wake unafanyika kwa awamu mbili.

Amesema awamu ya kwanza inahusisha ujenzi wa majengo tisa, likiwemo la utawala, madarasa, vyoo vya jumuiya, karakana za umeme na mabomba, uashi na useremala, upishi na ushonaji, nyumba ya mtumishi, jengo la mlinzi pamoja na jengo la umeme.

Amesema hadi sasa baadhi ya majengo yako katika hatua za mwisho za ukamilishaji, ikiwemo uwekaji wa mifumo ya umeme, maji, rangi na miundombinu ya maji taka.

“Mradi umepokea zaidi ya Sh777 milioni hadi sasa na hakuna mzabuni anayetudai. Utekelezaji unaendelea kulingana na upatikanaji wa fedha za mapato ya ndani ya halmashauri,” amesema.

Amesema awamu ya pili itahusisha ujenzi wa karakana ya ufundi magari, karakana ya uungaji vyuma, jiko, ukumbi wa chakula, maktaba, mabweni, stoo pamoja na nyumba za wakufunzi.

Pia, ameeleza ubora wa vifaa vinavyotumika katika ujenzi huo unasimamiwa kwa kufuata viwango vinavyotakiwa, huku saruji, nondo, kokoto, mchanga na tofali vikikaguliwa na mamlaka husika kabla ya kutumika.

Naye, Mbunge wa Kilolo, Ritta Kabati, amesema mradi huo utakuwa chachu ya maendeleo kwa vijana wa wilaya hiyo kwa kuwapatia ujuzi wa kujiajiri badala ya kutegemea ajira rasmi pekee.

“Huu ni uwekezaji mkubwa kwa vijana wetu. Tunatarajia kuona wahitimu wengi wakipata stadi zitakazowawezesha kujitegemea na hata kuajiri wengine,” amesema.

Mmoja wa wananchi wa Kata ya Mtitu, Moses Mpwani, amesema chuo hicho kitawaondolea vijana wa Kilolo adha ya kusafiri umbali mrefu kutafuta mafunzo ya ufundi stadi.

“Chuo hiki kitakuwa msaada mkubwa kwa vijana wetu. Wengi watapata ujuzi wa kujiajiri na kuanzisha shughuli za uzalishaji, jambo litakalosaidia kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira,” amesema.

Ziara ya Kihongosi mkoani Iringa inaendelea na anatarajiwa kuhitimisha Juni 21, 2026 katika Wilaya ya Mufindi.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports