RAIS WA NAMIBIA AWASILI KWA ZIARA YA KITAIFA NCHINI TANZANIA – Habari Mpya

Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah, amewasili nchini kwa Ziara ya Kitaifa ya siku tatu kuanzia tarehe 19 hadi 21 Juni 2026, kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam, Mhe.…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah, amewasili nchini kwa Ziara ya Kitaifa ya siku tatu kuanzia tarehe 19 hadi 21 Juni 2026, kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam, Mhe. Dkt. Nandi-Ndaitwah alipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Serikali. Katika mapokezi hayo pia alikuwepo Balozi wa Jamhuri ya Namibia nchini Tanzania, Mhe. Gabriel Sinimbo.

Ziara hiyo inafanyika katika kipindi ambacho Tanzania na Namibia zinaendelea kuimarisha uhusiano wao wa kihistoria uliojengwa katika misingi ya mshikamano wa harakati za ukombozi wa Afrika, urafiki wa muda mrefu na ushirikiano wa karibu katika nyanja mbalimbali za maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Akiwa nchini, Mhe. Rais Nandi-Ndaitwah anatarajiwa kufanya mazungumzo ya uwili na mwenyeji wake, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa lengo la kuimarisha zaidi ushirikiano katika sekta mbalimbali zenye manufaa kwa wananchi wa Tanzania na Namibia. Viongozi hao pia wanatarajiwa kushuhudia utiaji saini wa hati mbalimbali za makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Ziara hii ya kwanza ya Kitaifa ya Rais Nandi-Ndaitwah nchini Tanzania tangu alipoingia madarakani inaashiria dhamira ya pamoja ya Tanzania na Namibia ya kuendeleza ushirikiano wa kimkakati, kuimarisha diplomasia ya uchumi, pamoja na kukuza biashara na uwekezaji kwa manufaa ya pande zote mbili.

Ziara hii pia inatarajiwa kutoa fursa ya kuenzi historia ya ushirikiano wa ukombozi kati ya Tanzania na Namibia, huku ikifungua ukurasa mpya wa ushirikiano katika nyanja mbalimbali za maendeleo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho cha wananchi wa mataifa hayo mawili.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports