Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Richard Abwao amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime ameithibitisha Mwananchi leo Jumamosi, Julai 20, 2026 kuhusu kifo cha ofisa huyo alikuwa cheo cha Kamishna Msaidizi wa Mwandamizi.
“Ni kweli aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandamizi Richard Abwao amefariki dunia leo 20.6.2026 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa anapatiwa matibabu,”
“Taratibu zingine mtajulishwa baadaye,” amesema Misime.
Enzi za uhai wake, Abwao amewahi kuhuduma katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu kabla ya kuhamishiwa mkoani Tabora.
Endelea kufuatilia Mwananchi

















