Watu saba wafariki dunia katika ajali mbili Geita, Kahama

Kahama/Geita. Watu saba wamepoteza maisha na wengine 14 kujeruhiwa katika ajali mbili tofauti za barabarani zilizotokea ndani ya siku mbili katika mikoa ya Shinyanga na Geita, huku mwendokasi na uzembe wa madereva vikitajwa kuwa chanzo kikuu cha matukio hayo. Ajali moja imetokea leo Juni 20, 2026 katika eneo la Wendele, Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga,…

admin Avatar

by

2 minutes

Read Time

Kahama/Geita. Watu saba wamepoteza maisha na wengine 14 kujeruhiwa katika ajali mbili tofauti za barabarani zilizotokea ndani ya siku mbili katika mikoa ya Shinyanga na Geita, huku mwendokasi na uzembe wa madereva vikitajwa kuwa chanzo kikuu cha matukio hayo.

Ajali moja imetokea leo Juni 20, 2026 katika eneo la Wendele, Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, ambapo watu sita wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa, baada ya basi la Kampuni ya OG Classic kugongana na lori aina ya Tata lililokuwa likitoka Kahama kwenda Geita, na kisha kupinduka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi amesema uchunguzi wa awali unaonyesha dereva wa basi hilo alikuwa katika mwendo mkali na alijaribu kulipita lori lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari za kutosha.

“Akiwa katika mwendokasi aligonga ukingo wa barabara, akarudi kugonga tela la lori na kisha basi kupinduka,” amesema Magomi.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, waliopoteza maisha ni wanaume wanne na wanawake wawili ambao hadi tunachapisha taarifa hii walikuwa hawajatambuliwa, huku miili yao ikihifadhiwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama.

Amesema majeruhi watano wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini, huku dereva wa basi hilo, Chacha Bosco (35), akidaiwa kutoroka baada ya ajali na sasa anatafutwa na polisi ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Wakati huohuo, mtu mmoja amefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa katika ajali nyingine iliyotokea Juni 19, 2026 katika Kijiji cha Nyamigota, Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro mkoani Geita.

Ajali hiyo ilihusisha basi la Kampuni ya Najmunisa lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Geita na gari aina ya Tata linalomilikiwa na Kampuni ya Manyama lililokuwa likitoka Mwanza kwenda Ngara, mkoani Kagera.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Geita, Kenneth Mwakasitu amesema chanzo cha ajali hiyo pia ni mwendokasi na kutokuzingatia tahadhari za usalama barabarani.

Amesema dereva wa basi la Najmunisa alijaribu kuipita bajaji iliyokuwa mbele yake bila tahadhari za kutosha, jambo lililosababisha kugongana na gari jingine lililokuwa likitokea upande wa pili wa barabara.

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Katoro, Yohana Kitutu, amesema kituo hicho kilipokea majeruhi tisa pamoja na mwili wa mwanaume mmoja aliyefariki dunia katika ajali hiyo.

“Marehemu ametambulika kuwa kondakta wa basi la Najmunisa mwenye umri unaokadiriwa kuwa kati ya miaka 30 na 35. Majeruhi wanne walitibiwa hapa Katoro na watano walihamishiwa Hospitali ya Katoro kwa matibabu zaidi,” amesema Kitutu.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports