Category: Habari
-

DC Mtatiro awapa watendaji siku 14 kutatua kero za wananchi
Shinyanga. Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro, amewapa watumishi wa Serikali katika Wilaya ya Shinyanga Vijijini siku 14 kukamilisha uchunguzi na kuwasilisha taarifa za kina pamoja na mapendekezo ya utatuzi wa kero zote zilizowasilishwa na wananchi katika Tarafa za Samuye na Nindo. Akizungumza leo Juni 16, 2026, Mtatiro amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha changamoto…
-

Taasisi zapewa somo ziwajibike kwa jamii
DODOMA; Mwenza wa Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, Mama Neema Nchemba amehimiza aaasisi za umma na binafsi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za kijamii kupitia utekelezaji wa programu za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR). Amesema hayo, Juni 16, 2026 katika hafla ya kukabidhi vifaa vya hospitali vilivyotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS)…
-

Mbinu kumlinda mtoto dhidi ya matumizi hasi ya teknolojia hizi hapa
Dar es Salaam. Wakati nchi za Afrika leo zikiadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika, wadau wa malezi, elimu na teknolojia wameonya kuhusu kuongezeka kwa matumizi hasi ya teknolojia miongoni mwa watoto, wakitaka hatua za haraka kuchukuliwa ili kuwalinda dhidi ya hatari zinazotokana na matumizi yasiyo salama ya mitandao na vifaa vya kidijitali. Siku ya Mtoto…
-

JESHI LA MAGEREZA LASHIRIKI MAADHIMISHO YA KITAIFA YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2026 – Habari Mpya
Na. Ssgt Mawazo Mtondo – Dodoma. Jeshi la Magereza kwa mara nyingine tena linashiriki kikamilifu kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2026 Maadhimisho ambayo ni moja ya Maazimio ya Umoja wa Afrika (AU). Hivyo, Jeshi la Magereza linawakaribisha wananchi wote wa Tanzania kutembelea Banda la Magereza katika Maadhimisho ya…
-

Aweso aivunja menejimenti ya Mwauwasa, aonya uzembe
Mwanza. Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameivunja Menejimenti ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (Mwauwasa) kutokana na kutoridhishwa na kiwango cha utoaji huduma ya majisafi na salama jijini Mwanza. Uamuzi huo umefuatia ziara ya kikazi aliyoifanya Waziri jijini Mwanza, ambapo amebaini uwepo wa changamoto za upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama…
-

MAGARI MABOVU 07 YAKAMATWA, MADEREVA WENYE LESENI ZILIZOISHA MUDA WACHUKULIWA HATUA-SONGWE. – Habari Mpya
Magari saba (07) yaliyobainika kuwa na ubovu mkubwa yameondolewa namba za usajili, mengine yakatozwa faini huku baadhi yakielekezwa kurekebisha kasoro mbalimbali za kiufundi, kufuatia operesheni maalumu ya ukaguzi wa magari yanayotoa huduma za usafiri wa abiria iliyofanywa na Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Songwe katika Wilaya ya Songwe na vijiji vyake, kwa lengo la…
-

Makada Chadema walivyohojiwa Polisi kuhusu maandamano
Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimedai kadhia ambayo viongozi wake wanakutana nayo ikiwamo kukamatwa au kuitwa polisi kuhojiwa ni matokeo ya tuhuma zilizotolewa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi kuwatuhumu kupanga maandamano. Chadema imelitaka Jeshi la Polisi kumwita kiongozi huyo wa CCM kumhoji…
-

VULLU AWASIHI WAZAZI KUIMARISHA MALEZI,HUKU AKIGUSIA HATARI KWA WATOTO WA KIUME – Habari Mpya
Na Mwamvua Mwinyi, KibahaJuni 16, 2026 Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani, Zainab Vullu, amewasihi wazazi na walezi kuimarisha malezi ya watoto kwa kuwajenga katika misingi ya maadili, hususan watoto wa kiume ambao kwa sasa wanakabiliwa na hatari zinazotokana na mazingira hatarishi na mmomonyoko wa maadili. Amesema taifa haliwezi kuwa na maendeleo endapo watoto wa…
-

Kauli za kukemea ubaguzi zatikisa Bunge, Baraza la Wawakilishi
Dar/Zanzibar. Mjadala wa kurushiana vijembe kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar umeibuka baina ya wabunge na wawakilishi hali ambayo imekemewa na baadhi yao kuwa inaweza kuhatarisha Muungano na mshikamano wa kitaifa. Wakichangia mjadala wa bajeti, baadhi ya wabunge wameonya kauli zinazotolewa na baadhi ya mawaziri upande wa…
-

Vijana wapewa mbinu za kuitumia AI kwa mtindo mwingine
Dar es Salaam. Tanzania imejipanga kujenga uhuru wa nchi kupitia teknolojia ya akili unde (AI) na siyo kuwa na akili unde inayotengeneza utegemezi. Hivyo, katika kuhakikisha hilo vijana wamatakiwa kuwa wabunifu kwa kuja na mifumo ya AI itakayotumika kusaidia biashara, ujasiriamali na fursa mbalimbali za ndani na nje ya nchi. Hayo yamebainishwa leo Jumanne, Juni…
Latest News
About the Author
Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

Search the Archives
Access over the years of investigative journalism and breaking reports
You May Have Missed







