Hivi hapa vipaumbele 7 bajeti viwanda na biashara 2026/27

DODOMA; Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga amewasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo mwaka 2026/27 ikiwa na vipaumbele saba. Akiwasilisha bajeti hiyo leo Mei 22, 2026, Waziri Kapinga ametaja kuwa ni kuendelea na utekelezaji wa miradi ya kielelezo na kimkakati ya Viwanda. “Kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma kwa kuboresha mazingira…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

DODOMA; Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga amewasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo mwaka 2026/27 ikiwa na vipaumbele saba.

Akiwasilisha bajeti hiyo leo Mei 22, 2026, Waziri Kapinga ametaja kuwa ni kuendelea na utekelezaji wa miradi ya kielelezo na kimkakati ya Viwanda.

“Kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma kwa kuboresha mazingira wezeshi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya kongani (Industrial Clusters)  na mitaa ya viwanda (Industrial Estates)  kwa ajili ya viwanda vidogo na vya kati;

“Kuchochea maendeleo ya viwanda na biashara kupitia ubunifu na matumizi ya teknolojia za kisasa, elimu na mafunzo ya ujuzi,” amesema.

Ametaja vipaumbele vingine ni kuimarisha upatikanaji wa fedha na mitaji kwa wajasiriamali na wazalishaji viwandani;

“Kuboresha mazingira ya biashara na kuchochea ukuaji wa Sekta binafsi; kuendelea na utafutaji wa masoko kwa bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini na:

“Kuanzisha na kuendeleza mawazo ya biashara na bunifu (Innovation and Business Hubs) kwa vijana kwa lengo la kuchochea uchumi,” amesema Wazri Kapinga.

 

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports