Katambi ataja vipaumbele vinane 2026/27

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi ametaja maeneo manane ya vipaumbele katika bajeti yake kwa mwaka 2026/27, ikiwamo kufanya tafiti za kubaini chanzo cha makosa mapya ya kihalifu na kuweka mikakati ya kukabiliana nayo. Katambi amesema hayo leo Jumatatu, Mei 25, 2026 bungeni Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi…

admin Avatar

by

2 minutes

Read Time

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi ametaja maeneo manane ya vipaumbele katika bajeti yake kwa mwaka 2026/27, ikiwamo kufanya tafiti za kubaini chanzo cha makosa mapya ya kihalifu na kuweka mikakati ya kukabiliana nayo.

Katambi amesema hayo leo Jumatatu, Mei 25, 2026 bungeni Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake ya Sh2.4 trilioni.

Kati ya fedha hizo Sh1.95 trilioni sawa na asilimia 80 ya bajeti yote ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh489.8 bilioni sawa na asilimia 20 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Amesema Serikali itaendelea kuwajengea uwezo watumishi na askari kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali yatakayoongeza weledi na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Wizara imepanga kuanza ujenzi wa ofisi ya makao makuu ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) jijini Dodoma, ofisi 31 za usajili wa wilaya pamoja na kituo cha mafunzo na matengenezo ya vifaa vya Tehama Kibaha.

Pia, amesema wizara itaendelea kuimarisha shughuli za uzalishaji mali kupitia kilimo, mifugo, viwanda na utunzaji wa mazingira, sambamba na kuboresha miundombinu ya vyombo vya usalama ikiwamo makazi ya maofisa, wakaguzi, askari na watumishi wasiokuwa askari.

“Tutaboresha upatikanaji wa vitendea kazi, ikiwamo vyombo vya usafiri na usafirishaji kwa vyombo vya usalama pamoja na matumizi ya Tehama katika huduma zinazotolewa na wizara na taasisi zake,” amesema Katambi.

Katika hatua nyingine, waziri huyo amesema wizara itaanza ujenzi wa nyumba salama kwa waathirika wa usafirishaji haramu wa binadamu jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia ajira, Katambi amesema kuanzia Julai 2025 hadi Aprili 2026 wizara imeajiri watumishi 10,238, ambapo Jeshi la Polisi limeajiri askari 5,650.

Amesema katika mwaka 2026/27, wizara inatarajia kuajiri watumishi wengine 10,919, huku Jeshi la Polisi likitarajiwa kuajiri askari 8,040.

Kwa upande wa mafunzo, amesema jumla ya watumishi 13,475 wamepatiwa mafunzo ndani na nje ya nchi katika kipindi hicho, huku Sh38.81 bilioni zikitengwa kwa ajili ya kuwapatia mafunzo watumishi 23,547 katika mwaka ujao wa fedha.

Pia, amesema watumishi 9,689 wamepandishwa vyeo kati ya Julai 2025 na Aprili 2026, wakati wizara ikitarajia kupandisha vyeo watumishi 23,089 katika mwaka 2026/27.

Katambi pia amesema wizara inaendelea kukamilisha mfumo wa kielektroniki wa upimaji wa utendaji kazi kwa maofisa, wakaguzi na askari wa vyombo vya usalama.

Amesema Sh1.43 bilioni tayari zimetumika katika mradi huo ambao umefikia asilimia 93 na unatarajiwa kukamilika Juni 2026.

Kwa mujibu wa waziri huyo, mfumo huo utasaidia kuboresha masuala mbalimbali ya kiutumishi, ikiwamo upandishaji vyeo, utoaji wa likizo na mafunzo.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports