Kijana aliyemkumbatia Rais Ruto jukwaani apewa ajira, walinzi hatarini

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi nchini Kenya limeanzisha uchunguzi maalumu dhidi ya kikosi cha walinzi wa Rais wa Kenya, William Ruto baada ya kijana mmoja (jina halijawekwa wazi), kufanikiwa kupenya ulinzi na kumfikia kiongozi huyo wakati wa hafla ya shukrani iliyofanyika katika eneo la Ganze, Kaunti ya Kilifi Mei 24, 2026. Tukio hilo lililoteka…

admin Avatar

by

2 minutes

Read Time

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi nchini Kenya limeanzisha uchunguzi maalumu dhidi ya kikosi cha walinzi wa Rais wa Kenya, William Ruto baada ya kijana mmoja (jina halijawekwa wazi), kufanikiwa kupenya ulinzi na kumfikia kiongozi huyo wakati wa hafla ya shukrani iliyofanyika katika eneo la Ganze, Kaunti ya Kilifi Mei 24, 2026.

Tukio hilo lililoteka hisia za Wakenya wengi lilitokea wakati Rais Ruto alipokuwa akizungumza katika hafla ya kumpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana, Fikirini Jacobs ambapo kijana huyo alifanikiwa kuvuka ulinzi akiwa ameshika Biblia na kumkumbatia rais mbele ya mamia ya wananchi.

Katika taarifa  iliyotolewa na Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Kenya, jeshi hilo limeeleza kuwa tukio hilo ni uvunjifu wa usalama wa taifa na haliwezi kuvumiliwa licha ya vikosi vya usalama kuchukua hatua za haraka kudhibiti hali hiyo.

Katika taarifa yake, IGP Douglas Kirocho amesema tayari ameunda timu maalumu kufanya uchunguzi wa kina kuhusu namna kijana huyo alivyoingia hadi eneo la Rais pamoja na tayari yamefanyika mabadiliko ya haraka kwa kikosi cha ulinzi ili kuziba mianya ya kiusalama.

“Tukio lolote linalohusisha usalama wa mkuu wa nchi ni suala nyeti la usalama wa taifa na litashughulikiwa kwa uzito,” imesema taarifa hiyo.

Hata hivyo, wakati mamlaka zikiliona tukio hilo kama la kihalifu na tishio la usalama na kuanza kuwachunguza walinzi wa Rais, kijana huyo ameibuka kuwa gumzo nchini humo baada ya kuripotiwa kupewa kazi katika Mamlaka ya Bandari Kenya (KPA).

Kwa mujibu wa taarifa zilizosambaa kutoka nchini humo na picha zilizochapishwa na John Macharia, kijana huyo amepewa nafasi hiyo ya kazi baada ya kujieleza kuwa aliamua kuvuka ulinzi akiwa na Biblia iliyokuwa imehifadhi wasifu wake (CV) kwa matumaini ya kupata msaada kutoka kwa Rais huyo.

“Nimekuwa nikitafuta kazi kwa muda mrefu na niliamua kuchukua hatua hii ili Rais anionyeshe huruma,” amenukuliwa kijana huyo akisema baada ya tukio hilo.

Katika tukio hilo, Rais Ruto aliwaamuru walinzi wake wasimdhuru kijana huyo na badala yake kumsikiliza kabla ya kuahidi kumsaidia, akimtaja kama kijana jasiri.

“Huyu kijana ana ujasiri. Tutamsaidia,” alisema Rais Ruto mbele ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo.

Hatua ya kijana huyo kupewa kazi imezua mjadala mpana nchini humo na mitandaoni, huku baadhi ya wananchi wakisifu huruma ya Rais na wengine wakieleza wasiwasi kuhusu udhaifu wa mfumo wa ulinzi wa viongozi wa kitaifa hilo.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports