Mahita ataja kinachoisibu polisi, wadau wasema…

Dar es Salaam. Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Omary Mahita amesema miongoni mwa changamoto zinazolikabili jeshi hilo zinatokana na kuingiliwa na wanasiasa, hali inayoweza kuwafanya askari kutenda kinyume na misingi ya sheria na taaluma zao (PGO). Katika ufafanuzi wake kuhusu hilo, Mahita amerejea enzi za uongozi wake ndani ya jeshi hilo, akisema alipewa maelekezo…

admin Avatar

by

5 minutes

Read Time

Dar es Salaam. Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Omary Mahita amesema miongoni mwa changamoto zinazolikabili jeshi hilo zinatokana na kuingiliwa na wanasiasa, hali inayoweza kuwafanya askari kutenda kinyume na misingi ya sheria na taaluma zao (PGO).

Katika ufafanuzi wake kuhusu hilo, Mahita amerejea enzi za uongozi wake ndani ya jeshi hilo, akisema alipewa maelekezo na wanasiasa mbalimbali, lakini alikataa na kuishia kutekeleza ya mamlaka zinazopaswa kumwelekeza kwa mujibu wa sheria.

Mahita aliliongoza Jeshi la Polisi kwa takriban miaka 10 kuanzia Mei 1996 hadi Machi 2006. Alihudumu chini ya uongozi wa Rais Benjamin Mkapa (hayati) na mwanzoni mwa utawala wa Jakaya Kikwete ambaye ni Rais mstaafu wa Awamu ya Nne.

Kiongozi huyo wa zamani wa jeshi hilo, anaeleza hayo katika kipindi ambacho, kumekuwa na malalamiko ya baadhi ya wananchi, wanasiasa na wanaharakati kuhusu utendaji wa polisi.

Kutokana na malalamiko hayo, mwaka 2023, Rais Samia Suluhu Hassan aliunda Tume ya kuangalia mifumo ya haki jinai na ikapendekeza mageuzi ya mfumo na muundo wa jeshi hilo. Tume ilitaka liitwe huduma za kipolisi badala ya Jeshi la Polisi.

Mapendekezo ya mageuzi hayo kwa mujibu wa tume hiyo, yalitokana na kubaini jeshi hilo linatumia nguvu kupita kiasi, linakamata bila kufuata sheria, udhaifu wa upelelezi na utunzaji duni wa vielelezo.

Hata hivyo, baadhi ya mageuzi ikiwemo mabadiliko ya jina na muundo wa Jeshi la Polisi bado hayajatekelezwa kikamilifu, huku mageuzi yakiendelea kujadiliwa.

Mkuu huyo wa Polisi mstaafu, ameeleza hayo katika mahojiano aliyofanya hivi karibuni na Kituo cha Televisheni ya mtandaoni ya M&S Podcast.

Wanasiasa wanavyoingilia Jeshi la Polisi

Mahita amesema changamoto katika utendaji kazi wa jeshi hilo, alipata shida kutoka kwa wanasiasa waliokuwa wakitaka kumpa maelekezo ya kufanya kazi zake, akifichua kuwa aliyakataa na kubaki na msimamo wake.

Amesema hali hiyo pia inaathiri utendaji wa jeshi hilo hali inayofanya askari kufanya kazi zao tofauti na misingi ya sheria iliyoandikwa kwenye misingi mikuu ya jeshi hilo (PGO).

“Nilipata shida sana na wanasiasa. Polisi anapokea maelekezo ya Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu basi. Hata Waziri wa Mambo ya Ndani hana mamlaka kuniamrisha kazi, ndiyo maana kipindi changu alipata shida,” amesema.

Ili Jeshi la Polisi liondokane na vikwazo vya kiutendaji linavyokabiliana navyo, amesema linapaswa kuzingatia misingi ya sheria za utendaji wake na kujiepusha kutekeleza maelekezo ya wanasiasa katika ukamataji wa watu.

“Wazingatie misingi, waache kutumiwa na wanasiasa. Jeshi la polisi linaongozwa na Sheria zake zilizoandikwa kwenye PGO,” amesema.

Alipoulizwa kuhusu ukatili wake alipokuwa IGP, Mahita alikiri hilo, akifafanua aliutumia kusimamia nidhamu ya jeshi hilo na kuhakikisha kazi zinaenda kwa ufanisi.

Amesisitiza kuna wakati mazingira ya kazi ya kipolisi yanahitaji msimamo na mipaka ya wazi kati ya viongozi na wasaidizi wao.

“Ukicheza na mbwa utaingia naye hata msikitini, hata nyumbani kwako. Hawa wasaidizi wako wakishakujua watakuchezea kama babu yao,” amesema.

Ili Jeshi la Polisi liondokane na vikwazo vya kiutendaji linavyokabiliana navyo, amesema linapaswa kuzingatia misingi ya sheria za utendaji wake na kujiepusha kutekeleza maelekezo ya wanasiasa katika ukamataji wa watu.

“Wazingatie misingi, waache kutumiwa na wanasiasa. Jeshi la polisi linaongozwa na Sheria zake zilizoandikwa kwenye PGO,” amesema.

Licha ya ukali wake, Mahita amesema katika utekelezaji wa majukumu yake, hakuruhusu matumizi ya silaha za moto badala yake alielekeza matumizi ya mabomu ya machozi na baruti kutuliza ghasia.

Alipoulizwa kuhusu harakati za vijana wanaoibuka na madai mbalimbali nchini, Mahita amewasihi watumie busara kudai haki zao, ikiwemo kuwasilisha malalamiko kwenye Wizara ya Vijana iliyoanzishwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Wadau wazikumbuka enzi zake akiwa IGP

Mbunge wa zamani wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini, amemtaja Mahita kuwa miongoni mwa wakuu wa Jeshi la Polisi waliokuwa wakali na wakatili hasa dhidi ya viongozi wa siasa kutoka upinzani.

“Kama alivyosema mwenyewe alikuwa mtu katili sana wa ukatili usiofuata sheria. Sasa kukuta mtu wa cheo hicho anakuwa katili ni kwamba anakiuka sheria inayotawala mifumo ya siasa zetu.

“Nchi yetu ni ya vyama vingi na vipo huru kisheria kufanya kazi zake, lakini yeye hakuthamini hilo na aliwahi hadi kuwatuhumu Chama cha Wananchi (CUF) kuwa waliingiza contena la visu nchini lakini halijawahi kuonekana mpaka leo,” amesema Selasini ambaye wakati huo alikuwa kada wa NCCR Mageuzi kisha akahamia Chadema, akaenda NCCR- Mageuzi na hivi karibuni amerudi tena Chadema.

Kwa upande wa Mbunge wa zamani wa Bukoba Vijijini (Chadema), Alfred Rwakatale amekumbushia Mahita alivyopambana na maandamano ya vyama vya siasa katika kipindi chake.

“Mtu hupimwa kwa matendo yake si kwa kauli anazozungumza. Mimi nimekuwa kwenye siasa za upinzani wakati wa uongozi wa Mahita, kuna kipindi chama chetu cha CUF kikiwa na nguvu sana, tuliitisha maandamano.

“(Mahita) alitoa tamko kutuzuia na kwamba tukifanikiwa kuandamana atajiuzuru kiti chake. Lakini tulifanya maandamano ya amani tukafanikiwa hadi tukafika mwisho tukaongea na wanahabari na hakujiuzuru, kwa hiyo unaweza kupima alikuwa kiongozi wa namna gani,” amesema.

Mwanahabari mkongwe aliyekuwa mmoja wa wabunge wa mwanzo kutoka vyama vya upinzani enzi hizo, Ndimala Tegambwage amesema kipindi cha uongozi wa Mahita kulishuhudiwa mivutano ya polisi na wanasiasa kama ilivyo sasa.

“Kipindi chake ilikuwa ni mapambano kati yake na wanasiasa, mvutano wake na CUF ulifikia hatua ukaunda misemo maarufu ya ‘Ngangari na Ngunguli’. CUF Walipoanza kujiita ngangari, naye alisema kama wao ni ngangari basi mimi ni ngunguri,” amesema.

Akitaja athari za polisi kutozingatia PGO, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Anna Henga amesema inafungua milango kwa wanasiasa wasio waaminifu kutumia jeshi hilo kwa masilahi yao binafsi.

“Ni kweli kuna changamoto ya PGO kufuatwa. Kwa mfano kwenye PGO suala la maandamano inapaswa tu taarifa itolewe kwa polisi siyo kuomba ruhusa.

“Lakini hii inatafsiriwa kama kuomba ruksa sababu ni kuwa siasa na uchu wa madaraka imeingilia sana utendaji wa polisi, inatumika kama kichaka cha wanasiasa wasio waadilifu kujifichia,” amesema.

Kwa upande wake, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Benson Bagonza amekosoa utendaji unaolalamikiwa kwa jeshi la polisi katika kumaliza malalamiko dhidi yake, akisema ukatili ni kinyume cha sheria za utumishi wa jeshi hilo.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports