‘Lipeni kodi ya ardhi kuepuka kuepuka kufutiwa umiliki’

DODOMA; Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Leonard Akwilapo, ametoa rai kwa wamiliki wote wa ardhi nchini kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao wa msingi wa kulipa kodi ya pango la ardhi kwa wakati ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria, ikiwemo kufutiwa umiliki wa ardhi husika.‎‎Dk Akwilapo amesema kuwa kutolipa kodi ya pango la…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

DODOMA; Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Leonard Akwilapo, ametoa rai kwa wamiliki wote wa ardhi nchini kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao wa msingi wa kulipa kodi ya pango la ardhi kwa wakati ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria, ikiwemo kufutiwa umiliki wa ardhi husika.

‎Dk Akwilapo amesema kuwa kutolipa kodi ya pango la ardhi ni kosa linaloweza kuathiri hata uwezo wa mtu kukopesheka katika taasisi za fedha pamoja na kupoteza sifa za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi nchini.

‎“Napenda kuwafahamisha Watanzania wote kuwa kutokulipa kodi ya pango la ardhi ni kosa ambalo linaweza kukufanya ukakosa sifa ya kukopesheka katika taasisi za fedha, na vilevile kukosa sifa za kugombea nafasi za uongozi ikiwemo udiwani na ubunge,” amesema Dk Akwilapo.

‎Waziri huyo ameyasema hayo leo Mei 28, 2026, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka wa fedha 2026/2027 bungeni jijini Dodoma.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports