Dar es Salaam. Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imeifuta kesi ya madai ya mgawanyo wa rasilimali usio sawa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baina ya Bara na Zanzibar.
Kesi hiyo ya madai namba 8323 ya mwaka 2025 ilifunguliwa na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa Chadema, Said Issa Mohamed na wajumbe wawili wa Bodi ya Wadhamini wa Chadema kutoka Zanzibar, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu (marehemu kwa sasa).
Leo Alhamisi, Mei 28, 2026, Jaji wa Mahakama Kuu, David Ngunyale ameifuta kesi hiyo baada ya kuridhika kuwa hati ya madai ina kasoro kwani haielezi mgogoro huo yaani madai ya ukiukwaji wa sheria katika mgawanyo wa rasilimali uliodaiwa na walalamikaji ulianza lini.
Wadaiwa katika kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Hamidu Mwanga, Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam ni Bodi ya Wadhamini Waliosajiliwa wa Chadema na Katibu Mkuu wa chama hicho.
Endelea kufuatilia Mwananchi















