Matumaini mapya 150 wakipewa miguu bandia bure

Unguja. Mapinduzi mapya ya yanatarajia kuanza visiwani Zanzibar kwa watu waliokatwa miguu kupatiwa viungo hivyo bandia bure. Faraja hiyo inakuja kupitia Mradi wa Zanzibar 100 Limb Project ambao ni matokeo ya ushirikiano kati ya taasisi ya Naya Qadam Trust ya Uingereza na Zanzibar Global Health and Education Foundation (ZGHEF). Akizungumza na Mwananchi kuhusu hatua hiyo…

admin Avatar

by

2 minutes

Read Time

Unguja. Mapinduzi mapya ya yanatarajia kuanza visiwani Zanzibar kwa watu waliokatwa miguu kupatiwa viungo hivyo bandia bure.

Faraja hiyo inakuja kupitia Mradi wa Zanzibar 100 Limb Project ambao ni matokeo ya ushirikiano kati ya taasisi ya Naya Qadam Trust ya Uingereza na Zanzibar Global Health and Education Foundation (ZGHEF).

Akizungumza na Mwananchi kuhusu hatua hiyo jana Jumamosi, Mei 30, 2026, Katibu wa ZGHEF, El’Jabir Shao amesema shughuli hiyo inatarajia kuendeshwa kwa mwezi mmoja kuanza Juni mosi hadi Julai mosi Katika Hospitali ya Wilaya ya Mbuzini Unguja.

“Katika mpango huo tunatarajia kutoa miguu bandia kwa watu wasiopungua 150 bure, hii ni kwa mara ya kwanza kufanyika jambo kubwa kama hili katika visiwa hivi ambapo itakuwa faraja kwa watu hao,” amesema.

Kwa mujibu wa Shao, watu wote wenye mahitaji ya miguu bandia watapatiwa huduma hiyo lakini wanatakiwa kujisajili mapema ili kurahisisha upatikanaji wa miguu hiyo, mtu atatakiwa kupimwa kabla ya kupatiwa kulingana na ulemavu alionao.

Amesema mbali na kutoa miguu hiyo, pia mradi huo utajikita kuwafundisha mafundi wa ndani ili huduma hiyo iwe indelevu kwa watu wenye mahitaji.

“Muhimu hapa zaidi huduma zote za vipimo na uwekaji wa viungo bandia zitatolewa bure bila malipo, kwa hiyo ni faraja kubwa,” amesema  

Hatua hiyo inalenga kuwasaidia na kupiga hatua kuelekea maisha ya kujitegemea badala ya kutegemea wengine kisa kukosa baadhi ya viungo.

Mratibu wa mradi huo, Zarina Jafferji mzaliwa wa Zanzibar anayeishi nje ya nchi, amesema Wazanzibari wenye changamoto hiyo sasa watapata fursa ya kurejea katika hali zao za kawaida.

Amesema katika nia yake ya kutaka kuwasaidia Wazanzibari wasiokuwa na uwezo, ametumia gharama kubwa lakini anasukumwa na uzalendo wa kusaidia nchi yake.

Muhimili wa kitaalamu wa mradi huu ni taasisi ya Naya Qadam iliyoanzishwa na Dk Viquar Qurash; Daktari bingwa wa upasuaji wa mifupa nchini Uingereza  baada ya tetemeko la ardhi nchini Kashmir, alivumbua teknolojia ya viungo bandia vinavyotumia vifaa rafiki kama raba ili kuwasaidia wasio na uwezo.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports