Tume ya Mipango yabainisha vipaumbele 12, mikakati ya utekelezaji Dira 2050

Dar es Salaam. Ukiwa umebaki mwezi mmoja kuanza kwa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 (Dira 2050), Tume ya Taifa ya Mipango imeeleza vipaumbele 12 vitakavyofanyiwa kazi huku ikiainisha maeneo muhimu yanayohitaji msukumo wa kipekee ili kuleta mageuzi. Hayo yamebainishwa leo Jumapili Mei 31, 2026 Ikulu jijini Dar es Salaam na…

admin Avatar

by

5 minutes

Read Time

Dar es Salaam. Ukiwa umebaki mwezi mmoja kuanza kwa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 (Dira 2050), Tume ya Taifa ya Mipango imeeleza vipaumbele 12 vitakavyofanyiwa kazi huku ikiainisha maeneo muhimu yanayohitaji msukumo wa kipekee ili kuleta mageuzi.

Hayo yamebainishwa leo Jumapili Mei 31, 2026 Ikulu jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo wakati akitoa mrejesho wa kikao cha Tume hilo kilichokaa Mei 26, 2026 chini ya mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan.

Dira ya Taifa ya 2025 inatarajiwa kwisha muda wake Juni 30, 2026, hivyo kikao hicho cha kwanza mwaka huu, kimetengeneza mazingira ya kuanza kwa utekelezaji wa Dira 2050 pamoja na mikakati mingine ya utekelezaji wake. Dira 2050 itaanza Julai 1, 2026.

Akizungumza na vyombo vya habari, Profesa Kitila amezitaja sekta za kipaumbele ni pamoja na kilimo, viwanda na ujenzi, madini na nishati, utalii, michezo na sanaa, ubunifu na maudhui ya kidijitali na miliki, ardhi na maendeleo ya miji.

Sekta nyingine ni pamoja na biashara na uwekezaji, elimu, hifadhi ya jamii, kazi na ustawi wa jamii, uchumi wa buluu, sayansi, teknolojia, ubunifu na uchumi wa kidijitali.

“Tume ya Taifa ya Mipango ilielekeza kuwa Sekretariati ya Tume ijielekeze na kujikita katika kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo.

Aidha, katika kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo, Mwenyekiti wa Tume alielekeza kuwa, wakati ambapo Tume haikutani katika vikao vya kawaida chini yake, wajumbe wa Tume watajigeuza kuwa Ofisi ya Usimamizi wa Utekelezaji wa Mipango (Delivery Bureau) na vikao vyake vitasimamiwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ambaye ni Waziri Kitila,” amesema.

Waziri huyo amesema Tume ya Taifa ya Mipango ilielekeza kukamilishwa kwa haraka kwa majadiliano kati ya Serikali na wawekezaji kuhusu miradi ya kimkakati ya uwekezaji inayotarajiwa kujenga msingi ya kukuza uchumi na kuchochea ajira kama sehemu muhimu ya utekelezaji wa Dira 2050 na Mpango wa Nne wa Taifa wa Maendeleo ya Miaka Mitano (2026/27 – 2030/31).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 Mei 31, 2026 Ikulu, Dar es Salaam.

Katika kikao hicho cha Tume, Profesa Kitila amesema kilijadili na kuidhinisha miongozo na mikakati ya utekelezaji wa Dira 2050 ikiwamo; mwongozo wa kitaifa wa mipango. mwongozo huu utaongoza wizara, idara, mamlaka za serikali za mitaa na mwongozo wa kitaifa wa uidhinishaji miradi ya maendeleo. Tume imepewa jukumu la kuidhinisha miradi yote kabla ya kwenda wizara ya fedha kulipiwa.

Mingine ni mwongozo wa kitaifa wa ufuatiliaji na tathmini na uwajibikaji ambao ndio mwongozo unaotoa viasharia vya upimaji, na mkakati wa mawasiliano ya kimkakati katika utekelezaji wa Dira 2050 ili kuuwezesha umma kujua utekelezaji huo.

“Tunaanza kutekeleza Dira 2050 tukiwa na nyenzo zote muhimu ambazo hazikuwepo wakati tunaanza utekelezaji wa dira ya 2025. Kwa hiyo tumepiga hatua na kwa mara ya kwanza, Dira ilipelekwa bungeni na kuidhinishwa na wabunge,” amesema Profesa Kitila.

Amesema Tume hiyo imeidhinisha, pia, maeneo muhimu yanayohitaji msukumo wa kipekee kuleta mageuzi. Mambo hayo ni mageuzi katika maeneo ya utawala na utumishi wa umma, mageuzi katika uwekezaji na uzalishaji ambapo changamoto kubwa imekuwa ni tija ndogo katika uzalishaji. Pia, mageuzi katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kimazingira.

“Jumla kutakuwa na viashiria 206 ambavyo vitatumika kupima utekelezaji Dira na mafanikio yake ili kuleta matokeo yaliyotarajiwa,” amesema Profesa Kitila wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Vilevile, Waziri Kitila amesema Tume imeelekeza kuharakisha mazungumzo na wawekezaji katika miradi mikubwa ya kimkakati nchini. Ameitaja miradi hiyo kuwa ni mradi wa Liganga na Mchuchuma, mradi wa magadi soda wa Engaruka, mradi wa kuchakata gesi kuwa kimiminika (LNG) na mradi wa Kabanga nickel.

“Miradi hii inachelewa kwenye majadiliano kwa sababu ya msimamo wa Serikali wa kutaka bidhaa zisipelekwe nje ya nchi bila kuongezwa thamani,” amesema waziri huyo.

Kuhusu nafasi ya wananchi katika utekelezaji wa Dira 2050, Profesa Kitila amesema wanashiriki kwa kuifahamu Dira yenyewe na kufanya kazi kwa bidii wakijua kwamba hiyo ndiyo njia ya kufanikisha utekelezaji huo.

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa kuhusu Maelezo ya Tume ya Taifa ya Mipango juu ya kuanza utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 uliofanyika leo Mei 31, 2026 Ikulu, Dar es Salaam.

Poa, amesema wananchi wanashiriki kwa kuwakosoa viongozi wao ambao utendaji wao unakwamisha utekelezaji wa Dira hiyo kwa ufanisi, na hivyo kusababisha mipango iliyowekwa isifikiwe.

“Wananchi ndiyo wamewaweka viongozi madarakani, kwa hiyo wanashiriki kwa kuwawajibisha pale wanapoona mipango haiendi vizuri,” amesema Profesa Kitila.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (Tiseza), Giliard Teri amezungumzia wanayofanya kuvutia uwekezaji ikiwa ni pamoja na kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji hasa kwa kuboresha sheria na muundo wa taasisi.

Pia, amesema wamekuwa wakiwahakikishia wawekezaji usalama ili wawekeze na kuwa na uhakika na mitaji yao hapa nchini. Amesema wanasisitiza diplomasia ya uchumi kwa kushirikiana na balozi za Tanzania zilizopo kwenye mataifa mengine duniani.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports