Bajaji iliyobeba wanafunzi zaidi ya 10 yanaswa, dereva afungiwa leseni

Moshi. Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limemkamata na kumfungia leseni kwa miezi mitatu dereva wa bajaji aliyekuwa amebeba wanafunzi zaidi ya 10 wa shule mbalimbali za msingi katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro. Akizungumzia tukio hilo leo Juni 2, 2026, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kilimanjaro, Nassoro Sisiwaya amesema baadhi ya…

admin Avatar

by

2 minutes

Read Time

Moshi. Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limemkamata na kumfungia leseni kwa miezi mitatu dereva wa bajaji aliyekuwa amebeba wanafunzi zaidi ya 10 wa shule mbalimbali za msingi katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Akizungumzia tukio hilo leo Juni 2, 2026, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kilimanjaro, Nassoro Sisiwaya amesema baadhi ya madereva bajaji katika mkoa huo wamekuwa na tabia ya kujaza wanafunzi kwenye vyombo hivyo vya moto, hali inayohatarisha maisha ya wanafunzi.

“Kumekuwa na mtindo wa bajaji kujaza abiria hasa asubuhi watoto wanapokwenda shuleni, kuna bajaji mmoja tumemkamata leo akiwa na wanafunzi wengi. Tumemfungia leseni kwa muda wa miezi mitatu,” amesema Kamanda Sisiwaya.

Amewaonya madereva bajaji wenye tabia kama hizo kuacha tabia hiyo na kwamba kufanya hivyo kunaweza kuhatarisha maisha ya wanafunzi.

“Niwaonye madereva wote wa bajaji wenye tabia ya kujaza abiria na wanafunzi nyakati za asubuhi. Ni marufuku, wanapaswa kufuata sheria za usalama barabarani vinginevyo tutaendelea kufungia leseni na hatua kazi za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,” amesema Kamanda Sisiwaya.

Katika tukio jingine, jeshi hilo limemkamata dereva mmoja aliyekuwa akiendesha gari la wanafunzi wa shule ya msingi mkoani humo akiwa amelewa kwa kiwango cha kilevi cha 504 na kusababisha kufungiwa leseni ya udereva kwa miezi sita.

Mmoja wa madereva aliyekamatwa akiwa amelewa akipiimwa kilevi na mmoja wa askari wa kikosi cha usalama barabarani Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

“Tunaendelea na operesheni zetu za kawaida ambapo tunakamata makosa yote hatarishi ikiwemo ulevi, mwendokasi kwa vyombo vyote vya moto hapa mkoani kwetu,” amesema Kamanda Sisiwaya.

Ameongeza kuwa: “Leo tumekamata madereva mbalimbali wakiwa na ulevi ambapo tumemkamata dereva mmoja wa gari la shule, akiwa na kilevi cha 504, hiki ni kilevi cha juu sana na tumemfungia leseni yake kwa muda wa miezi sita akafanye kazi nyingine.”

Amewataka wamiliki wa shule za msingi na sekondari mkoani humo kuhakikisha wanawakagua madereva wao asubuhi kabla ha kuchukua wanafunzi.

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports