Dar es Saalam. Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Ummy Mwalimu kuwa mshauri wa Rais katika masuala ya afya, ustawi wa jamii, wanawake na watoto.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumanne Juni 2, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, uteuzi huo unaanza rasmi mara moja.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi wa Ummy unalenga kuimarisha ushauri wa kimkakati kwa Rais katika sekta muhimu zinazogusa maisha ya wananchi, hususan afya ya jamii na ustawi wa makundi maalumu.
Ikumbukwe Ummy alikuwa Mbunge wa Tanga Mjini na Waziri wa Afya uteuzi kama waziri ulianza 2020 na kukoma 2023.
Endelea kufuatilia Mwananchi….















