Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mbeya Bi. Erica Yegella amebainisha kwamba katika ziara hiyo wameambatana na baadhi ya watendaji pamoja na madiwani mbali mbali kwa lengo la kuweza kwenda kujifunza mafunzo mbali mbali kwa kioindi cha siku nne ambayo yataweza kuwasaidia katika suala zima la utekelezaji wa majukumu yao ya kikazi ya kila siku.
Yegella amesema kwamba lengo kubwa la Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuwahudumia wananchi wake na kuleta chachu ya maendeleo na mabadiliko makubwa katika nyanja mbali mbali hivyo ana imani kwamba kufanyika kwa ziara hiyo kwa upande wa madiwani itawezamkuleta tija na mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kutokana na mafunzo ambayo watajifunza.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya BI. Aiddah Haule amesema kwamba mafunzo ambayo watayapata wakiwa katika visiwa hivyo vya unguja yeye pamoja na jopo la madiwani pamoja na mkurugenzi wapo yatakuwa ni mkombozi mkubwa katika kuleta mageuzi katika nyanja mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuwahudumia wananchi katika maeneo yao mbali mbali.












