MWENGE WA UHURU WAWASILI KONDOA,MIRADI YA BILIONI 3.9 KUKAGULIWA – Habari Mpya

Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 umewasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma ambapo jumla ya miradi 14 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.9 inatarajiwa kukaguliwa, kuwekwa mawe ya msingi pamoja na kuzinduliwa. Miradi hiyo inalenga kuboresha huduma za kijamii na kuongeza ustawi wa wananchi wa Wilaya ya Kondoa. Mwenge huo umepokelewa na Mkuu…

admin Avatar

by

1 minute

Read Time

Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 umewasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma ambapo jumla ya miradi 14 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.9 inatarajiwa kukaguliwa, kuwekwa mawe ya msingi pamoja na kuzinduliwa.

Miradi hiyo inalenga kuboresha huduma za kijamii na kuongeza ustawi wa wananchi wa Wilaya ya Kondoa.

Mwenge huo umepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Fatma Almas Nyangasa ukotokea Wilaya ya Bahi.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Wazo Michael Mwang’onda amewataka wazazi nchini kuwalea watoto wao katika maadili mema ili kujenga jamii yenye heshima na uwajibikaji.

Aidha, amewahimiza vijana kuwa wazalendo kwa nchi yao kwa kushiriki shughuli za maendeleo na kulinda tunu za Taifa.

Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 inasema; “Tanzania ni yetu sote, tushikamane kwa pamoja kuleta maendeleo.”

About the Author

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

Search the Archives

Access over the years of investigative journalism and breaking reports